Ray C Amwangukia Zamaradi Mketema, Awapasha Wema Sepetu Na Kajala.
Ray C na Zamaradi |
Ray anaonekana kupevuka kiakili na kifikra sana siku hizi ! kupitia
mtandao mmoja wa kijamii, star huyo wa muziki wa Bongoflava amewashauri
wasanii kuacahana na beef za kijinga badala yake waonyeshane upendo na
kuspotiana katika kazi.
Ray C pia hakusita kumuomba msamaha Zamaradi
Mketema ambaye walikwaruzana miezi michache iliyopita, huku pia aiwasihi
Wema Sepetu na Kajala kuonyeshana upendo kama awali na kusahau tofauti
zao
"Kiukweli huwa naumia sana ninapoona mastaa tunatumia muda
mwingi kulumbana na kugombana kwa mambo ya kipuuzi sana,mastaa wenzetu
wa Nigeria wanatushinda kwa mambo mengi sana sababu wao wanashirikiana
na kusapotiana katika mambo mengi sana na hata ukisikia wamepishana basi
ujue ni kwa ajili ya biashara tu na si vinginevyo! nilichogundua mimi
ni kwamba kumekuwa na makundi mbalimbali mitandaoni yanayokuza mambo na
kusapoti wasanii kulumbana mara Team Simba mara Team Nyani! naongea
kutoka. Moyoni kuwa watanzania tunasifika kwa kuwa na amani na upendo!
sasa iweje tena tuishi maisha ya kuchukiana na ugomvi badala ya kuishi
kwa amani?
Najua sisi wasanii tuna mashabiki wengi. na tunawapenda na nyie
mnatupenda kwahiyo mnatakiwa kutupatanisha tunapogombana na si
kutushabikia coz mnaposhabikia ugomvvi ndio mnapotufanya tupoteze muda
kulumbana badala ya kutumia huo muda kufanya kazi zetu za sanaa kwa
bidii tutangaze nchi yetu tunapoteza muda kulumbana,wenzetu wanaigeria
wako mbali sana kwa sababu wanasapotiana sana! wasanii tuache bifu za
kijinga na tutumie muda mchache tuliopewa na mola kufanya kazi zetu kwa
bidii tutangaze nchi yetu ili vizazi vijavyo virithi bidii zetu,na
naomba sana mashabiki wote msapoti mazuri tuyafanyayo"
Ray C pia hakusita kumuomba msamaha aliyekuwa hasimu wake Zamaradi
Mketema ambaye walidaiwa kumgombea Ruge miezi michache iliyopita na
kurushiana maneno mitandaoni
"Love u zama n sorry for everything keep doing wat u do best
@zamaradimketema n hey dogo langu @wemasepetu and my friend @new_kajala
tusameheane na tupendane na tupige kazi Africa watutambue bana!!!!!!"
Maoni
Chapisha Maoni