Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam. Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais. Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi? Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha. By iparamasa
Ujerumani imenyakuwa Kombe la Dunia kwa mara ya nne na kuwa timu ya kwanza ya Ulaya kulitwaa kombe hilo katika ardhi ya Amerika Kusini baada ya kuishinda Argentina goli moja kwa sifuri katika fainali Washangiliaji waliomimika kwa maelfu kuangalia mechi hiyo ya aina yake walikuwa wakiishangiria Argentina, huku zaidi ya raia 100,000 wa Argentina wakiripotiwa kumiminika nchini Brazil kupitia mpakani na baharini, lakini hilo halikuwadumaza Wajerumani. Mario Götze ndiye aliyeweka kimiani goli la kwanza na la pekee katika dakika 113 na hivyo kuiandika nchi yake kwenye kitabu cha historia ya ushindi wa Kombe la Dunia. Kwa mara ya kwanza Ujerumani ilishinda Kombe hilo mwaka 1954, kisha 1974 na 1990, wakati huo bado ikiwa imegawika kati ya mashariki na magharibi. Ushindi wa mara hii ni wa kwanza tangu mashariki na magharibi kurudi tena kuwa taifa moja la Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani. Ujerumani ndiyo timu ya kwanza ya Ulaya kushinda Kombe la Dunia katika ardhi ya Amerika y
Maoni
Chapisha Maoni