BREAKING NEWS : MUME WA CELINE DION AFARIKI DUNIA

Celine Dion na mumewe Rene Angelil enzi za uhai wake.
Las Vegas, Marekani
Rene Angelil, mume wa mwanamuziki mashuhuri duniani Celine Dion, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73, nyumbani kwao Las Vegas nchini Marekani baada ya kuugua saratani ya koo iliyomsumbua tangu mwaka 2000.
Bw Angelil pia alikuwa meneja wa Celine Dion, alimuoa mwaka 1994 na wakajaliwa watoto watatu.
Dion alichukua likizo kutoka kwenye muziki kwa vipindi viwili ili kumtunza Angelil baada kupatikana na saratani ya koo mwaka 2000.
Bw Angelil alizaliwa mjini Montreal mwaka 1942.

Celine Dion (kushoto) akiwa na wazazi wake pampja na Rene (kulia) mwaka 1982.
Baada ya kuwa meneja wa makundi kadha nchini Canada, aliombwa na wazazi wa Dion awe meneja wake mwanamuziki huyo alipokuwa na umri wa miaka 12 pekee.
Mwaka jana, Dion aliambia gazeti la USA Today kwamba alikuwa akijiandaa kwa kifo cha mumewe.
“Ikifika, itafika tu,” aliambia gazeti hilo Agosti 2015.
“Lakini kibarua change kikubwa kitakuwa kumwambia mume wangu kwamba tuko sawa. Nitawatunza na kuwalea watoto wetu. Utatutazama kutoka ulimwengu mwingine.”

Rene amemwachia mjane wake watoto waiwili mapacha Eddy na Nelson (waliobebwa, kwa sasa wana umri wa miaka mitano) na mtoto mwingine mkubwa, Rene Charles Jr. (aliyesimama kulia, kwa sasa ana umri wa miaka 1). Picha zimepigwa mwaka 2011.
Gazeti la Montreal Gazette linasema Bw Angelil aliweka rehani nyumba yake ili kupata pesa za kufadhili albamu ya kwanza ya mwanamuziki huyo.
Dion amerekodi albamu 25 studioni na ndiye mwanamuziki wa tano kwa kulipwa pesa nyingi zaidi, utajiri wake ukikadiriwa kuwa dola za kimarekani milioni 630 (sawa na euro milioni 437).
Mwaka 1999, wimbo wake My Heart Will Go On, uliotumiwa katika filamu ya Titanic, ulishinda tuzo mbili za Grammy.
Amekuwa akitumbuiza mara kwa mara katika ukumbi wa The Colosseum, Caesars Palace mjini Las Vegas tangu mwaka 2003.
Alianza tena kutumbuiza mashabiki wake mwaka jana baada ya kupumzika mwaka mmoja kumtunza Bw Angelil, ambaye aliacha kuwa meneja wake 2014.
PICHA NA DAILY MAIL

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.