Sakata la UDA Laanza upya
Wakati Serikali ikiendelea kuchunguza mikataba kati ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) kuhusu Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ametia pilipili kidonda kwa kuibua udanganyifu unaolizunguka shirika hilo. Kwenye ripoti yake ya mwaka wa fedha 2014/2015 aliyoitoa bungeni Jumatatu, CAG Profesa Mussa Assad amebainisha kwamba Dart ilifanya makubaliano na msimamizi wa uendeshaji, Uda-RT kutoa huduma ya mpito ya usafiri kwa kutumia mabasi 76 yenye vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba. Tofauti na makubaliano hayo, Uda ilinunua mabasi 140 ambayo yalikuwa na nembo ya Uda-RT badala ya Dart kinyume na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba. Meneja wa Miundombinu wa Dart, Mhandisi Mohamed Kuganda alisema wenye ta...