VITUO VYA MWENGE, MAKUMBUSHO KABLA NA BAADA YA MABADILIKO
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
KAMERA yetu leo imeongea na wadau kuhusu kuhamishwa kwa kituo cha mabasi ya daladala kutoka Mwenge kwenda Makumbusho ambapo malalamiko yanahusu umbali wa kituo hicho kutoka maeneo ya abiria wengi na ubovu wa miundo mbinu sehemu hiyo kama ukosefu wa vyoo, vifaa vya kutupia uchafu na mashimo kwenye barabara kituoni na zile zinazoingia hapo.
Malalamiko mengine ni kwamba kituo ni kidogo mno, hakina alama muhimu za kuonyesha mabasi yanakokwenda.
Wengi walitaka barabara za hapo ziwekwe lami, na wengine wakataka nauli ya kutoka Bagamoyo iongezwe kwani mabasi sasa hayaishii Mwenge bali Makumbusho.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni