Chuji aenda na maji, Kaseja kazi ipo
Chuji.PICHA|MAKTABA
- Lakini kipa Juma Kaseja bado shughuli yake ni pevu
Lakini kipa Juma Kaseja bado shughuli yake ni pevu.
Kaseja amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na nusu, uamuzi wake bado haujatolewa lakini anaweza kubaki.
Uamuzi wa Chuji ulitolewa katika kikao cha
viongozi hao kilichofanyika Ijumaa na Jumamosi kwa madai yao ya awali
kuwa mchezaji huyo ana utovu wa nidhamu ambao utawasumbua.
Habari za ndani ambazo Mwanaspoti imezipata ni
kwamba Chuji aliitwa na kupewa onyo kali akitakiwa kujirekebisha tabia
huku ikielezwa kwamba kocha mpya atakayeingia mkataba na Yanga ndiye
atatoa uamuzi wa mwisho juu ya kiungo huyo.
Lakini tayari uamuzi umetolewa kabla hata Maximo
ambaye enzi akiwa kocha wa Taifa Stars alionyesha misimamo ya waziwazi
wa kutovutiwa na tabia za Chuji.
“Chuji ana mkataba na Yanga, lakini tumekubaliana
kwamba atalipwa fedha zake za kuvunjwa mkataba wake, bado hajapewa
taarifa Chuji ila ukweli upo hivyo atapata timu nyingine kwani zipo
nyingi.
“Hata viongozi wenyewe waligawanyika kuhusu Chuji
kuna waliotaka abaki na wengine hawahitaji, hivyo maamuzi ya mwisho ni
kumwondoa kikosi,” alisema kiongozi huyo ambaye alitaka jina lake
lihifadhiwe mpaka hapo viongozi watakapotoa taarifa rasmi ya wachezaji
watakaoachwa.
Maoni
Chapisha Maoni