Baby Madaha : “Wema Sepetu Tuachie Na Sisi Huyo Diamond Tumfaidi “


Star wa filamu na muziki wa Bongoflava Baby Madaha anadaiwa kuwewesekea penzi la Diamond Platnumz na kumtaka Wema Sepetu awaachie na wao Diamond a.k.a Sukari ya warembo ili wafaidi kama anavyojiachia. 
Chanzo kimoja kilicho karibu na Baby Madaha ambacho pia kinafanya juu chini kuwika katika filamu kwa masharti ya kutotajwa jina lake kikizungumza na Swahiliworldplanet wiki iliyopita kilisema kuwa:
 
“Nawapa habari, Baby Madaha anamtaka Diamond hata kule kumponda kwenye media sio kwa dhati ni njia ya kumshawishi amtongoze. 
Staa wa filamu Bongo, Baby Madaha
Staa wa filamu Bongo, Baby Madaha

“Sikia nikwambie, katika Kill Awards (mwaka huu) Madaha alikuwa na lengo la kumbusu Diamond kwa stage lakini  alikuwa anamhofia Wema na Team Wema wangeweza kuja juu ikawa habari mpya…
 
“Anamtaka ila anashindwa tu kusema wazi, unajua Wema anambana sana Diamond, anataka Wema amwachie” kilisema chanzo hicho huku kikisisitiza kuwa kisitajwe jina lake .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA