Kigodoro Chamfanya Wema Sepetu Ashindwe Kuhudhuria BET Awards 2014.
WEMA |
Hata hivyo chanzo kimoja kilicho karibu na Wema na Aunty kimeipenyezea Guiji la habari kuwa moja ya sababu iliyomfanya Wema ashindwe kwenda BET Awards licha ya kueleza kuwa angehudhuria kupitia Instagram siku kadhaa nyuma ni kufanyika kwa sherehe ya rafiki yao mmoja maeneo ya Mwananyamala nyumbani kwa Aunty Ezekiel juzi, ambapo asingeweza kuwaacha mashosti zake hao peke yao pasipo sapoti yake katika shughuli hiyo. Kwa mujibu wa chanzo kilichoomba kutowekwa wazi jina lake walicheza sana ikiwemo muziki wenye mahadhi ya kigodoro ambayo ni ngoma/muziki uliyojipatia umaarufu siku za hivi karibuni kiasi cha "kuwawehusha" baadhi ya kinadada wa mjini.
"Wema hajaenda BET Awards alikuwa kwenye kigodoro Mwananyamala na kina Aunty, kuna rafiki yao anaitwa Imelda alipata mtoto ndo wakamfanyia sherehe. watu walikula, kunywa na kusaza, walichezajee ! kajala na wema walimaliza mgomgoro wao hapo, ntakutumia na picha pia ila usinitaje" kilisema chanzo hicho ingawa kilishindwa kutuma picha hizo kwa wakati mpaka tunaandika habari hii.
Katika tuzo za BET Awards Diamond hakuwa na team kubwa kama ilivyokuwa tuzo za MTV nchini S.Afrika
Wema na kina Kajala katika shughuli hiyo
Maoni
Chapisha Maoni