PICHA: Kikongwe auawa kikatili kwa kukatwa Shoka kichwani huko Kahama


Bibi mmoja Mkazi wa mtaa wa Nyahanga, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Rebeka Sengasenga (82), ameuawa kwa kukatwa na Shoka kichwani kwa kile kinachohisiwa kuwa ni imani za Kishirikina.
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo limetokea  jana asubuhi katika Mtaa wa Nyahanga, wilayani humo, ambapo Marehemu Rebeka alienda nyumbani kwa mtoto wake Bundala Sengasenga alikokuwa ameitwa na mke wa Bundala kusaidia kuanika Dengu.
Imeelezwa kuwa Merehemu Rebeka ambaye alikuwa akiishi kwa mwanae mkubwa Stanley Sengasenga katika mtaa huo alifika kwa Bundala  baada ya kuitwa na Magreth Richard ambaye ni mke wa Bundala kwa ajili ya shughuli hiyo.
1       
Katika maelezo yake Magreth amesema Mama mkwe wake Marehemu Rebeka alifikia sebuleni, na kwamba wakati yeye yuko nje, alimwona mtu ambaye hakuweza kumfahamu akitoka sebuleni hapo na kukimbia ndipo alipoangalia na kumkuta Rebeka ameuawa.
2
Taarifa za awali zimedai, kabla ya tukio hilo  Magreth ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi mjini Kahama kwa mahojiano alienda nyumba ya jirani kuazima Shoka, ambalo baadaye limekutwa kwenye shimo la maji taka nyumbani hapo.

Anayeshikiliwa akilia kwa uchungu ni Magreth anayehisiwa kuhusika na tukio hilo.
Anayeshikiliwa akilia kwa uchungu ni Magreth anayehisiwa kuhusika na tukio hilo.
Shoka hilo limepatikana baada ya mbinu za kiupelelezi za Jeshi la Polisi kuagiza gari la maji taka kuyavuta maji hayo baada ya majirani kudai hawajaona mtu aliyekimbia na shoka muda huo katika mwelekeo ambao Magreth ameelekeza.
Mwili wa Marehemu Bi Rebeka ukiondolewa eneo la tukio kupelekwa Mochwari
Mwili wa Marehemu Bi Rebeka ukiondolewa eneo la tukio kupelekwa Mochwari
 
Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku upelelezi ukiendelea.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA