MAUAJI MENGINE YA KUTISHA YATOKEA KENYA! POLENI WAKENYA
Kenya: Mauaji mengine yatokea Mpeketoni
Nchini Kenya wakati serikali ikiimarisha juhudi zake za kupambana na ukosefu wa Usalama ndani ya Taifa hilo,bado mashambulio zaidi yanaendelea kushuhudiwa katika sehemu mbali mbali za nchini humo.
Mauaji ya watu wengine watano usiku wa kuamkia leo katika eneo la Witu,kilomita chache tu kutoka Mpeketoni, ambako zaidi ya watu 60 waliuawa kinyama na watu wasiojulikana mapema wiki iliyopita, yanazidi kuzitia dosari mbinu hizi zinazotumiwa na vyombo vya usalama wa ndani katika kukomesha mauaji ya kiholela kwa Wakenya wasio na hatia. hivi sasa mahubiri yote ya kidini usiku imepigwa marufuku mjini humo mombasa . Mwandishi wetu eric Ponda ana ripoti zaidi. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Maoni
Chapisha Maoni