
Chris Brown akiwa mwenye uso wa furaha baada ya kuachiwa huru
Hatimaye hitmaker wa Loyal ‘Chris Brown’ ameachiwa huru
asubuhi ya leo tangu awekwe kuzuizini katikati ya mwezi machi baada ya
kukiuka kanuni za Rehab, ingawa kuachiwa huko kunatajwa kuwa ni kwa
muda mfupi kutokana na kukabilia na kibarua kingine cha kujibu mashtaka
ya kesi yake ya pili ya kumshambulia shabiki mjini Washington DC na
endapo atapatikana na hatia huenda akakumbwa na kifungo cha miezi 6
gerezani.
Akionyesha kila dalili za furaha, mwimbaji huyo hakuwa na
budi zaidi ya kumshukuru mwenyezi mungu kwa kumuwezesha kutoka nyuma ya
nondo za jela ya LA County na kisha kumalizia kwa kuwasabahi mashabiki
wake aliokuwa amewamisi kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
”Humbled and Blessed”, ”Back to the music and the Fans” na ”Thank You God” hizo zilikuwa baadhi ya tweets alizoandika Brown kwenye ukurasa wake wa twitter.
Mashabiki wa Chris Brown wakiwa wameshika mabango nje ya mahakama wakishinikizwa kuachiwa huru kwa jembe lao
Maoni
Chapisha Maoni