BILIONEA OPRAH WINFREY AZIDIWA KETE NA MKURUGENZI WA MICROSOFT KATIKA UNUNUZI WA TIMU YA LOS ANGELS CLIPPERS.
Steve Ballmer
Awali Oprah Winfrey, Antony Ressler, Steve Ballmer pamoja na mchezaji wa zamani wa Lakers Magic Johnson ndio waliotajwa kuwania nafasi ya kutaka kuinunua timu hiyo licha ya hapo baadae mambo kugeuka.
Oprah mwenye umri wa miaka 60 ambaye kwa sasa anarekodi kipindi kipya amesema kuwa ameshangazwa na hatua ya kuwekewa vikwazo yeye kama mwanamke kununua timu hiyo ya mpira wa kikapu na kufikiri sana juu ya suala hil.
Alinukuliwa akisema kwamba kiwango chake cha mwisho ni dola bilioni 2 ambapo amesema tangu aweke hadharani kukasirishwwa kwake na kitendo hicho amejisikia nafuu kiasi.
Timu ya Los Angels Clippers yenye wachezaji nyota kama vile Blake Griffin na Chris Paul ilikumbwa mgogoro majuma kadhaa yaliyopita baada ya mmiliki wake ‘Donald Sterling’ kumtolea matamshi ya kibaguzi mpenzi wake, hali iliyopelekea afungiwe na chama cha NBA kutojuhusisha kwa namna yoyote na timu hiyo kabla ya kushauriwa kuibiga bei.
Maoni
Chapisha Maoni