MBASHA: Maisha ya Jela hayafai kabisa.
Kufuatia Mahakama ya Ilala jijini Dar kumuachia kwa dhamaa Emmanuel Mbasha ambaye ni mume wa muimbaji wa nyimbo za Injili maarufu nchini Flora Mbasha anayekabiliwa na tuhuma nzito za kumbaka mdogo wa mkewe, inaelezwa kuwa siku moja tu aliyokaa mahabusu ilimfanya kubadilika muonekano kutokana na kudhoofika…..
Emmanuel Mbasha ambaye alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza juni 17 mwaka huu na kukosa dhamana kutokana na kushindwa kutimiza mashariti, alilazimika kutupwa mahabusu katika gereza la Keko, kabla ya juni 19 kupandishwa tena kizimbani ambapo aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti hayo….
Baadhi ya watu ambao walimshuhudia Mbasha katika viunga vya mahakama hiyo walioneklana kulengwa na machozi huku wengine wakitamka kwamba wanamuachia Mungu…..
Mume huyo wa Flora aliwasikitisha zaidi watu kutokana na kuwa na mawazo mengi huku miguuni akiwa amevaa malapa ambayo thamani yake haizidi sh. 2000 wakati katika hali ya kawaida huwa anavaa mavazi ya bei mbaya na kujiweka msafi muda wote…..
“Maskini Imma amevaa ndala na amekonda.Hakika yupo katika kipindi kigumu sana. Jela mtu hukonda siku moja tu.Jela siyo kuzuri hata hata kidogo,” alisema raia mmoja nje ya mahakama hiyo.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo Wilberforce Luhwago aliahirisha kesi hiyo hadi July 17 mwaka huu itakapo tajwa tena…..
Baada ya kuachiwa, Mbasha alitoka nje ya mahakama hiyo kwa kasi na kuingia kwenye gari kisha kutoweka eneo hilo….
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja kati ya ndugu wa Mbasha ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema kuwa mume wa mwanamuziki huyo aliwaambia hana hamu na jela,
“Mbasha alisema kuwa jela hakufai kabisa na alisisitiza kuwa asaidiwe kutoka kwa dhamana. Alisema siku moja aliyoishi mahabusu ni kama mwaka mzima,” alisema ndugu huyo.
Aidha ndugu huyo alisema kwamba kitendo cha Flora kutomtembelea mume wake ni cha kinyama na hakuna aliyekitarajia.
“Hakwenda kumuona mume wake.Kwa kweli jambo hili limetushangaza sana na kutuumiza sana, sijui mwisho wake utakuwa vipi lakini tunaamini yatakwisha, kwa uzuri au ubaya,” alisema.
Baadhi ya mahabusu ambao walikuwa selo moja na Mbasha katika gereza la Keko wamesema kwamba wamefurahi kuwa na nyota huyo kwani wamekuwa wakimsoma kwenye magazeti tu
Maoni
Chapisha Maoni