UWEZO WA MAREKANI KIJESHI WASHUKA, UKILINGANISHA NA CHINA NA URUSI!


Wanajeshi wa marekaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Jopo la wataalam lilichapisha uchanganuzi wa mkakati wa usalama wa rais Donald Trump.
Jukumu ambalo Marekani imechukua kwa miaka mingi sasa limetokana na uwezo wake wa kijeshi. Leo hatahivyo uwezo huo umekandamizwa katika maeneo fulani muhimu, ilisema ripoti hiyo.
Kuna changamoto za dharura ambazo ripoti hiyo inasema ni lazima ziangaziwe ili kupunguza uharibifu wa muda mrefu katika usalama wake wa kitaifa.
Bunge la Congress lilitoa wito kwa tume ya kimkakati kuhusu ulinzi nchini humo kufanya utafiti huru kuhusu mkakati wa kiusalama wa utawala wa rais Trump.
Tume hiyo iliongozwa na Eric Elderman, afisa wa zamani wa Pentagon wakati wa utawala wa raia George W Bush na mkuu wa zamani wa jeshi la wanamaji nchini humo Admirali Gary Roughhead.
Wote ni watu wenye ufahamu mkubwa kuhusu matumizi ya idara ya ulinzi mbali na kuwa wataalam katika Pentagon.
Usalama na ustawi wa Marekani unakabiliwa na hatari kubwa katika kipindi cha miongo kadhaa, ripoti hiyo ilisema.
Uwezo wa kijeshi wa Marekani umeshuka hadi kiwango kinachohatarisha.

Tishio la China na Urusi

Kuwasili kwa rais Trump katika ikulu ya Whitehouse kuanaingiliana na kubadilika kwa mahitaji na malengo ya kijeshi: mbali na operesheni dhidi ya uvamizi na vita dhidi ya ugaidi na kuangazia uwezekano wa kuzuka kwa vita dhidi ya washindani wake China na Urusi.
Hata wale wasio na ushindani mkubwa kama vile Iran na Korea kaskazini pia wanatoa changamoto mpya na zilizo hatari. Athari zake ni kubwa kwa jeshi la Marekani.
Katika maeneo kama Iraq au Afghanistan, kwa mfano, wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira ambayo hayana tishio la angani kwa majeshi yake, na hakuna changamoto kubwa (isipokuwa kijiografia) kwa mawasiliano yao, kama vile utumiaji wa GPS, nk.
Wakati huo huo, wapinzani - kama vile Uchina na Urusi - wamekuwa wakilichunguza jeshi la Marekani na wanaendelea kuimarisha, wakiongeza uwezo wao wa jadi mbali na kutafuta njia mpya za kukabili uwezo za Marekani katika maeneo ambayo imekuwa ikitawala.
Marekani inakabiliwa na jeshi la China lililoimarika katika bahari ya kusini mwa ChinaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ukweli ni kwamba , uingiliaji wa Urusi katika vita huko Ukraine ulionyesha uwezo wa kushangaza kuhusu uharibifu uliofanywa na silaha za Urusi, zilizohusisha uwezo wake wa kisasa, kurekebisha na kuharibu silaha za Ukrain na kuficha eneo ambalo la vikosi vya Urusi vilikuwa vikitekeleza operesheni zake
Katika idara nyingi , Marekani ina hatua kubwa kupiga ili kuafikia viwango hivyo.
Hiyo inamaanisha kurudisha nyuma na kuanzisha mkakati mpya, lakini pia ni zaidi ya hiyo.
Inahitaji juhudi kubwa kuendesha uvumbuzi na teknolojia muhimu: Akili bandia AI, mitandao ya kizazi kipya, nk, ambayo inaweza kutoa kipengee muhimu cha uwezo katika vita vya siku zijazo.
Ripoti hiyo ilionekana kama onyo.
Ilikuwa na malengo mazuri na hisia fulani za changamoto kubwa, lakini pia ilikuwa na mbinu zenye kutilia shaka juu ya jinsi ya kuyakabili, na kimsingi bila rasilimali za kutosha kutekeleza jukumu hilo.
Xi Jinping amechukua hatua ya kuliimarisha jeshi la ChinaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kuna zaidi ya mapendekezo 30 yenye maelezo.
Hapa hapa mambo muhimu zaidi ya ripoti hiyo:
  • Kuzingatia matumizi katika hisa za Marekani na washirika wake dhidi ya Uchina barani Asia na dhidi ya Urusi barani Ulaya
  • Kupunguza hatari ya kutegemea vifaa vilivyoingizwa kutoka nje, kwa mfano, kutoka China
  • Kudumisha uwepo wa kijeshi wa Marekani katika Mashariki ya kati, hata baada ya kuwashinda wapiganaji wa Kiislamu wa Islamic State.
  • Kuongeza vikosi vya Marekani ili viweze kupigana vita viwili, kwani kwa sasa wana uwezo wa kukabilina na adui mmoja pekee.
  • Kutoa mizinga zaidi, makombora ya masafa marefu na ufundi wa silaha.
  • Kuuanzisha vitengo zaidi vya uhandisi na vile vya ulinzi wa angani
  • Kuimarisha idadi ya manuwari za wanamaji mbali na uchukuzi wao wa majini.
  • Kuimarisha idadi ya wanamaji na sio kupunguza idadi hiyo.
Wanajeshi wa Nato ni miongoni mwa vikosi vya NATOHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ripoti hiyo inapunguza ukubwa wa mkakati kuhusu ulinzi wa kitaifa ambao umetolewa na Rais Trump. Lakini hii sio hati ya mapinduzi, kwani inashirikisha maono ya kimkakati ambayo yanaelezea fikra za Pentagon.
Inaangazia vidokezo ambapo mipango rasmi haifai au haifanyi vizuri.
Ni wito kwa matumizi ya juu lakini pia kwa gharama thabiti zaidi. Na inasisitiza kuhusu umuhimu wa jukumu hilo.

Ni kubwa

Jeshi la Marekani bila shaka sio jeshi lisilo na nguvu.
Lakini kuingia katika biashara ya silaha za hali ya juu itakuwa ghali. Ujuzi wa jadi utalazimika kutolewa tena. Changamoto mpya, zitalazimika kuchambuliwa na kuelekezwa.
Ripoti ya tume hiyo inafikiria kwamba Marekani itasalia kuwa mtendaji mkuu wa kijeshi kote ulimwenguni ikiwemo barani Ulaya, eneo la Asia Pacific na Mashariki ya Kati.

Diplomasia

Lakini baadhi ya matatizo makuu yanatoka nje ya jeshi: katika viwanda na katika nyanja pana ya diplomasia. Kipindi kirefu cha utawala wa jeshi la Marekani wakati wa Vita baridi kilitokana na msingi wa kisayansi na viwanda vyake ambapo hakuna mtu angeweza kushindana naye.
Hatua zilizopigwa katika utafiti wa anga na teknolojia nyingine zinazohusiana na sekta ya jeshi zimekuwa zikifanywa na raia .
Mambo ni tofauti sana leo. Ni utafiti wa raia - katika kompyuta, vifaa vya elektroniki - ambao unaendesha maendeleo ya kiteknolojia. Na Marekani - ingawa ina uwezo mkubwa haipo pekee.
Wanajeshi wasiotambulika walichukua eneo la CrimeaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
China hususan, inawekeza rasilimali kubwa katika teknolojia ambazo siku moja zinaweza kuipatia fursa katika uwanja wa vita vya karne ya 21. Utandawazi umechanganya uchumi wa China na Marekani kwa njia ambazo zinaweza kuwa hatari kwa usalama wa Marekani.
Fedha zinahitaji kuwekezwa vizuri zaidi. Programu za upatikanaji wa silaha zinahitaji kuharakishwa na kuwezeshwa zaidi mbali na kuzipatia kasi njia za hatua za kiteknolojia .
Matumizi ya Marekani yanapita yale ya wapinzani wake wakubwa kijeshi lakini bado haijapata kile inachostahili kulingana na matumizi yake.
Kuna pia kipengele cha kidiplomasia.
Marekani haijifunzi kupigana pekee bali na washirika wake. Rais Trump amezingatia nyanja moja tu ya uhusiano huu: ugawanaji wa majukumu, hitaji la nchi za NATO haswa kufanya matumizi zaidi kuhusu usalama wao wa pamoja.
Lakini rais Trump amewakosea washirika wake jinsi alivyofanya
Muungano wa mataifa ya Atlantic wenyewe umedhoofishwa kisiasa, hata ikiwa vikosi zaidi vya Marekani vitapelekwa Ulaya ili kuimarisha ulinzi wao dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Sera ya Trump ya kigeni imewakosea washirika wakeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Uhusiano wa muungano huo unaweza kupona wakati utawala wa Trump utakapoisha.
Katika kiwango cha kisiasa, wanahitaji kulishwa, na katika ngazi ya kijeshi, hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa hatua zozote za Marekani katika teknolojia haziyafanyi mataifa mengine washirika kiuhisi vigumu kushirikiana na taifa hilo.

Mtazamo mpya?

Pengine changamoto kubwa iliyotolewa na ripoti hii ni wito wake kwa Marekani kuchukua mchakato mpya wa usalama kwa jumla.
Zote Urusi na Uchina, kulingana na hati hiyo, zina mikakati ambayo inaunganisha zana zote za nguvu za kitaifa. Marekani nayo inahitaji kuwa na mpangilio kama huo.
Bila shaka, hii ni muhimu wakati ambapo changamoto zinaongezeka.
Hati hiyo inaitaka serikali kuchukua mchakato mpya wa usalama kwa jumlaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Hatuishi tena katika ulimwengu ambao kuna tofauti ya wazi kati ya amani na vita.
Nafasi kati ya maswala hayo imejawa na changamoto na mitego mingi: habari, mauaji ya kisiasa, shambulio la mitandaoni na shughuli za jeshi za vikosi au washirika ambao kitambulisho chao hupotea kulingana na muda.
Kukabili ukweli huu mpya na ulio mgumu unahitaji mkakati mpya, mawazo mapya na zana mpya.
Lakini pia inahitaji mtazamo mpya kutoka kwa serikali swala ambalo inaweza kuwa vigumu zaidi kuafikia.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.