BEIJING DAXING: UWANJA MKUBWA WA KIMATAIFA WA NDEGE CHINA WAFUNGULIWA, HATARIIII!


Beijing Daxing airportHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUwanja mkubwa wa ndege China una ukubwa wa viwanja 98 vya soka
Uwanja mpya mkubwa wa ndege wa kimataifa China wenye thamani ya $11bn umefunguliwa siku chache kabla ya maadhimisho ya miaka 70 nchini humo.
Uwanja wa ndege wa Daxing uliopo katika mji mkuu Beijing umefunguliwa rasmi na rais Xi Jinping hii leo.
Uwanja uliopo hivi sasa Beijing ni wa pili wenye shughuli nyingi duniani baada ya ule wa Atlanta, kwa mujibu wa wa baraza la viwanja vya ndege.
lakini maafisa wanasema uwanaj mpya wa ndege unahitajika kuondsha shinikizo kutoka kwenye uwanja huo wa kimataifa Beijing unaojaa watu kupita kiasi.
Uwanja wa ndege wa Daxing- unaotajwa kuwa na kiingilio kikubwaduniani katika jengo moja - unatarajiwa kuwapokea idadi kubwa ya wasafri milioni 170 wanaotarajiwa kukaribishwa mjini humo kufikia 2025.
Kwa mujibu wa shirika la serikali, Global Times, ndeg saba za ndani zilitarajiwa kuanza shughuli katika uwanja huo mpya hii leo Jumatano. ndege ya kwanza - China Southern Airlines A380 - iliondoka mwendo wa saa 16:23 kwa saa ya huko.
Na ndege za kimataifa zikiwemo British Airways, Cathay Pacific na Finnair tayari zimetangaza njia mpya kwenda Daxing.
Uwanja huo wa ndege, ulio takriban 46km kusini mwa Tiananmen Square, uliundwa na msanifu mijengo maarufu Zaha Hadid.
Kutokana na ufunguzi huo, Beijing imejiunga na makundi ya miji yakiwemo New York na London, ambayo ina viwanja viwili vya kimataifa.
zaidi ya abiria milioni 100 wamewahi kupitia Beijing Capital, uliofunguliwa mnamo 1958.
Daxing Airport in June 2019Haki miliki ya pichaAFP
Image captionDaxing Aiport mnamo Juni 2019
Beijing Daxing International Airport during a construction completion ceremony on June 30, 2019Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUliundwa na msanifu mijengo maarufu Zaha Hadid.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.