LISA LI: NYOTA MASHUHURI FEKI, AUMBUKA BALAAAA!


Lisa Li ameanikwa mitandaoni na mwenye nyumba aliyopangwaHaki miliki ya pichaPEAR VIDEO
Image captionLisa Li ameanikwa mitandaoni na mwenye nyumba aliyopangwa
Mshawishi maarufu wa mtandao nchini China ameangaziwa kwa kuishi maisha ya "uwongo", baada ya mwenye nyumba aliyopangisha kufichua maisha yake halisi yanayotofautiana na muonekana anaonadi mtandaoni.
Kanda ya video iliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha nyumba ya Lisa Li - Mwanablogu maarufu aliye na mashabiki milioni 1.1 - ikiwa na uchafu uliozagaa kila sehemu- ikiwa ni pamoja na vyakula vilivyooza na kinyesi cha mbwa.
Tangu kanda hiyo iliposambazwa mitandaoni Bi Li ameomba msamaha.
Kwanini Bi Li ni mashuhuri?
Lisa Li anafahamika China kama "wang hong", ama "Mtu mashuhuri", katika mtandao maarufu wa Sina Weibo.
Akaunti yake, sawa na ya vijana wa Kichina ambao ni watu mashuhuri wa mtandaoni, inaonesha jinsi anavyopenda starehe kwa kusafiri katika maeneo ya kuvutia, kuhudhuria hafla tofauti na kula vyakula vya hali ya juu.
Lakini tangu mwenye nyumba aliopanga kumuanika mtandaoni amepata umaarufu mwingine tofauti kabisa (maisha yake ya faraghani ambayo ameweka siri).
Watumiaji wa mtandao wa Weibo walishangazwa na uchafu uliozagaa kila sehemu katika nyumba ya LiHaki miliki ya pichaTHE PAPER
Image captionWatumiaji wa mtandao wa Weibo walishangazwa na uchafu uliozagaa kila sehemu katika nyumba ya Li
Mwenye nyumba alifanya nini?
Baada ya Lisa Li kupuuza simu alizompigia, mamilioni ya watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Weibo walimtazama mwenye nyumba aliyetajwa na vyombo vya habari kama Bi Chen, akioneshana mazingira machafu ya nyumba ya Lisa.
Bi Chen aliiambia Pear Video kuwa hata wataalamu wa kufanya usafi wamekataa kusafisha nyumba hiyo na kuongeza kuwa mpangaji alikuwa anadaiwa maelfu ya yuan ambazo hajalipa kupata huduma muhimu wanazopewa wapangangaji wengine.
Chen amesema hakua na budi kupiga ripoti polisi ili kukoa mali yake na kupata fedha anazoda.
Video inayoonesha jinsi sakafu ya Li ilivyochafu ilipata umaarufu mitandaoniHaki miliki ya pichaPEAR VIDEO
Image captionVideo inayoonesha jinsi sakafu ya Li ilivyochafu ilipata umaarufu mitandaoni
Lakini Chen alipata umaarufu baada ya kuonesha ukurasa wa Weibo wa mpangaji wake kwa kituo hicho, akisema: "Huyu ni mtu mashuhuri sana mtandaoni na anafuatiliwa na watu milioni moja."
Aliaimbia Pear Video katika mahojiano ya kipekee akisema "mwanamke mrembo" lakini muonekano wake ni tofauti na "uvundo" na uchafu uliopo nyumbani kwake.
Bi Li amesemaje?
Lisa Li na mwenye nyumba wasalimianaHaki miliki ya pichaPEAR VIDEO
Image captionBi Li (Kushoto) alikutana na mwenye nyumba (Kulia) kuomba msamaha na kuahidi kushughulikia suala hilo
Baada ya mamiliaoni ya watu kuona kanda ya video ya nyumba hiyo Bi Li alijitokeza na badala ya kutoa taarifa katika mtandao wa kijamii aliamua kukutana na mwenye nyumba ana kwa ana na kuomba msamaha.
"Nakubali nimekosea kutokana na tukio hili," alimwambia Bi Chen. Alinaswa katika kanda ya video akimsalimia mwenye nyumba.
Alielezea sababu za kutokuwepo kwake katika mtandao maarufu wa habari -The Paper, akisema ilitokana na kazi nyingi.
Pia alisema alikuwa mgonjwa na alipotoka hospitali alienda safari ya kikazi.
Aliongeza kuwa hivi karibuni alipokea ujumbe mwingi katika WeChat na huenda hakuona ya mwenye nyumba.
"Sasa nitasafisha … nitapasafisha usiku huu," aliiambia The Paper.
Mashabiki wa Bi Li wanasemaje?
Bi Li akisafisha nyumba yakeHaki miliki ya pichaPEAR VIDEO
Image captionBi Li akisafisha nyumba yake
Kanda inayomuonesha Bi Li akizoa kinyesi cha mbwa kwa kutumia kifagio cha nyumbani imewagutusha mashabiki wake huku baadhi yao wakimkejeli mtandaoni.
Zaidi ya watumiaji 60,000 wametoa maoni katika ukurasa wake, na wengi wao wamesema wataacha kumfuatilia huku wakiimuita "feki".
Baadhi yao pia wamehoji ukweli wa mahajiano yake katika vyombo vya habari.
Mashabiki wake pia wamegundua kuwa amebadilisha anuani yake katika mtandao wa kijamii na kufuta posti za awali.
Bi Li aliiambia The Paper kwamba aliona ujumbe kutoka kwa mwenye nyumbaHaki miliki ya pichaTHE PAPER
Image captionBi Li aliiambia The Paper kwamba aliona ujumbe kutoka kwa mwenye nyumba
Hii sio mara ya kwanza visa kama hivi vinashuhudiwa nchini China.
Taifa hilo limekua likiwashinikiza raia wake mashuhuri kuwajibika katika jamii.
Mwezi Julai vlogger mmoja raia wa China alikejeliwa sana mitandaoni baada ya hitilafu ya kimitambo wakati akifanya live-stream( matangazo ya moja kwa moja mtandaoni) kumuonesha kuwa mwanamke wa wa umri wa makamo tofauti na jinsi alivyojinadi mtandaoni kuwa mwanamke kijna.
Baadhi ya watu mashuhuri mtandaoni walikiuka "maadili" wamefungwa jela kwa muda mfupi.
Mwezi Oktoba mwaka 2018, Yang Kaili, kinara mashuri wa live-stream aliye na mamiliaoni ya mashabiki, alizuiliwa kwa siku tano kwa kukashifu wimbo wa taifa.
Mtandao Huya wa kupeperusha matangazo ya moja kwa moja mtandaoni ulifuta tangazo hilo na kumpiga marufuku,ukisema kuwa mitandao ya kurusha matangazo yanastahili kuzingatia sheria kikamilifu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.