SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LATANGAZA KUSAMBAZWA KWA BOEING 787S KWA SAFARI ZAKE TOFAUTI MWAKA 2016

 


Shirika la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa kwa Falme za kiarabu limetangza kuanzisha mipango ya kurusha ndege aina ya boeing 787s kwa safari za kwenda Dusseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg kwa mwa mwaka 2016.

Matarajio ya kuwasili kwa ndege hizo mpya aina ya Boeing 787s ni ndani ya miezi saba ijayo, kuanzia Mei 2016, ndege hizo “Dreamliners” zenye uwezo wa kubeba abiria 299 zitaanza kutoa huduma kwenda Dusseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg kutoka Abu Dhabi zikichukua nafasi ya ndege zinazotumika sasa.

Kwa sasa Shirika la ndege la Etihad lina ndege tano tu aina ya 787s ambazo zinafanya safari zake kati ya Brisbane, Washington, Singapore na Zurich moja kwa moja kutoka Abu Dhabi. Matarajio ya Shirika hilo ni kuongeza zaidi ya Boeing 66 ndani ya miaka kadhaa ijayo ambapo ndege hizo aina ya “Dreamliners”zitakuwa ndege rasmi za shirika hilo kwa masafa marefu.

James Hogan, ambaye ni Rais na afisa mkuu wa shirika la ndege la Etihad alisema: “Tangu kuanzishwa kwa ndege aina ya 787 ya kwanza katika huduma za kibishara mnamo februari mwaka huu, tumekuwa tukipata maoni mazuri kutoka kwa abiria wetu  ambayo yamekuwa kama alama ya ubora wa hali ya juu katika kanda na dunia nzima.

“Kuanzia mwezi Mei mwakani, shirika la ndege la Etihad litazindua ndege mpya Boeing 787 aina ya dreamliners zitakazotumika rasmi badala ya hizi zilizopo kwa safari za masafa marefu ambapo zitatoa fursa kwa abiria wetu kupanda ndege za teknolojia mpya.

“Abiria na wateja wetu wa siku hizi wanapenda kusafiri bila kero wala pirika pirika kwenye usafiri wa viwango vya juu, wanataka chaguo zuri zaidi na bei nafuu. Hivi ndivyo vigezo vyao vikuu katika kuchagua na sisi hapa Etihad tunajitahidi kufikia matarajio hayo kwa tafiti na uvumbuzi wa aina mbalimbali kama vile kuleta ndege mpya na kuendelea kuboresha njia zetu za usafiri.

Ndege hizi mpya aina ya 787-S zitajumuisha ubunifu wa ndani ya kabini 28 za “business studios” na siti 271 za “economy smart” zikiwa na utulivu, burudani na uwezo wa kuunganishwa kwa mawasiliano zikiwa angani. Upambaji wa ndani na mwanga vimesukwa zaidi kwa ubunifu wa kiarabu zikiendana na ubunifu mpya wa kutoka “Abu dhabi” ulioletwa na shirika la ndege hili katika uzinduzi mpya mwaka jana.

Ratiba ya Boeing 787 kwenda DUSSELDORF, kuanzia Mei mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):



Ndege Na.
   

Inaanzia
   

Inaondoka
   

Itawasili
   

Muda wa kufika
   

Mizunguko

EY0023
   

Abu Dhabi (AUH)
   

02:15
   

Dusseldorf (DUS)
   

07:20
   

Kila siku

EY0024
   

Dusseldorf (DUS)
   

11:50
   

Abu Dhabi (AUH)
   

20:25
   

Kila siku



Ratiba ya Boeing 787 kwenda PERTH, kuanzia Juni Mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):



Ndege Na.
   

Inaanzia
   

Inaondoka
   

Itawasili
   

Muda wa kufika
   

Mizunguko

EY0486
   

Abu Dhabi (AUH)
   

22:25
   

Perth (PER)
   

13:50 siku inayofata
   

Kila siku

EY0487
   

Perth (PER)
   

15:40
   

Abu Dhabi (AUH)
   

23:10
   

Kila siku



















Ratiba ya Boeing 787 kwenda SHANGHAI, kuanzia Agosti Mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):



Ndege Na.
   

Inaanzia
   

Inaondoka
   

Itawasili
   

Muda wa kufika
   

Mizunguko

EY0862
   

Abu Dhabi (AUH)
   

21:55
   

Shanghai (PVG)
   

11:10 siku inayofata
   

Kila siku

EY0867
   

Shanghai (PVG)
   

00:30
   

Abu Dhabi (AUH)
   

06:25
   

Kila siku











Ratiba ya Boeing 787 kwenda ISTANBUL, kuanzia Agosti 1 2016 (muda wa Abu dhabi):



Ndege Na.
   

Inaanzia
   

Inaondoka
   

Itawasili
   

Muda wa kufika
   

Mizunguko

EY0097
   

Abu Dhabi (AUH)
   

09:05
   

Istanbul (IST)
   

13:10
   

Kila siku

EY0096
   

Istanbul (IST)
   

14:25
   

Abu Dhabi (AUH)
   

20:00
   

Kila siku























Ratiba ya Boeing 787 kwenda JOHANNESBURG, kuanzia Novemba Mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):



Ndege Na.
   

Inaanzia
   

Inaondoka
   

Itawasili
   

Muda wa kufika
   

Mizunguko

EY0604
   

Abu Dhabi (AUH)
   

10:00
   

Johannesburg (JNB)
   

16:40
   

Kila siku

EY0603
   

Johannesburg (JNB)
   

19:40
   

Abu Dhabi (AUH)
   

06:00 next day
   

Kila siku















                                                         - Mwisho-

Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad

Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.

Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na  airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.