ROSTAM AZIZI KATIKA MSIBA MKUBWA


ALIYEKUWA mbunge wa Igunga,   Rostam Aziz, (CCM),  amefiwa na baba yake Aziz Abdulrasool (73) jijini Dar es Salaam jana asubuhi.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu Oysterbay jana, mtoto wa pili wa marehemu, Akram Aziz, alisema baba yake alifariki saa 12 asubuhi ikiwa ni saa mbili tu baada ya kurudishwa nchini kutoka Ufaransa alikuwa anatibiwa.


“Baba amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani,tumemrudisha nchini jana saa 10 alfajiri kutoka Ufaransa, lakini ilipofika saa 12:30 alifariki dunia.

“Baada ya kugundulika kuwa na saratani, alianza  matibabu Nchini Ufaransa  na Kurudi hapa Nyumbani…Mara ya mwisho baba alipelekwa nje miezi miwili iliyopita, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya akaomba tumrudishe nyumbani ili awe karibu na ndugu na mafariki zake,”alisema Akram.

Marehemu alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu, saa 10 jioni jijini Dar es Salaam na amewacha wajane watatu,watoto 17 na  wajukuu  nane.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.