TRUMP AKIRI KWAMBA ANACHUNGUZWA MAREKANI

Trump akiri kwamba anachunguzwa Marekani 16 Juni 2017 Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Donald Trump amekana tuhuma kwamba maafisa wake walishirikiana na maafisa wa Urusi Rais wa Marekani Trump amethibitisha kwamba anachunguzwa yeye binafsi kutokana na hatua yake ya kumfuta kazi mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai la Marekani FBI James Comey. Kupitia Twitter, Bw Trump amekariri kwamba uchunguzi unaoongozwa na mwendesha mashtaka maalum kuhusu tuhuma kwamba maafisa wa Urusi waliingilia uchaguzi wa mwaka 2016 ili kumfaa Trump hauna msingi. Ni mara ya kwanza kwa Bw Trump kuzungumzia taarifa kwenye magazeti kwamba anachunguzwa kwa tuhuma za kuhujumu mifumo ya haki kwa kumfuta kazi Bw Comey. Waziri mkuu Australia amkejeli rais wa marekani Donald Trump Sessions: Sikufanya mikutano ya siri na maafisa wa Urusi Trump aisifu Saudi Arabia kwa kuitenga Qatar Awali, taarifa kwenye vyombo vya habari Marekani vilikuwa vimeripoti kwamba wasaidizi wake pamoja na watu waliojitolea kusaidia katika kundi lake la mpito wameamrishwa kuhifadhi nyaraka zote kuhusiana na uchunguzi huo wa madai kuhusu Urusi. Taarifa zinasema mawakili wa maafisa hao wa Trump wametakiwa kuhifadhi nyaraka zote zinazohusiana na Urusi, Ukraine na washauri wengine kadha wa kampeni. Kuna makundi kadha yanayofanya uchunguzi, kundi moja likiongozwa na mkurugenzi wa zamani wa FBI Robert Mueller, ambayo yanachunguza iwapo maafisa wa Trump walishirikiana na maafisa wa Urusi wakati wa kampeni. Bw Trump amekana tuhuma hizo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.