Mchezaji wa Azam Farid Mussa Afaulu Majaribio Nchini Hispania....

WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa Malik (pichani kulia) wa klabu ya Azam ya Dar es Salaam amefaulu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.
Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa anayefuatilia majaribio ya mchezaji huyo Hispania, amesema kwamba CD Tenerife sasa inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na Azam FC juu ya kumnunua mchezaji huyo.

“Tunatarajia kuanza mazungumzo nao juu ya suala la Farid, ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili. Sasa tunasubiri ofa yao rasmi, kisha Bodi ya Ukurugenzi itajadili na kutoa maamuzi,”amesema Bakhresa.

Kwa upande wake, Farid amefurahia matokeo hayo na kusema haikuwa kazi nyepesi kwake kuweza kuwaridhisha maofisa wa benchi la ufundi la Tenerife.

“Kwa kweli nimefurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa kufuzu majaribio, ila haikuwa kazi nyepesi, mpira wa Ulaya mgumu,”amesema.

Awali, Farid ilikuwa apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga, kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.