Bajeti 2019: Tanzania na Uganda zapendekeza kodi kwa mawigi na visodo

Waziri wa fedha Tanzania' ametangaza kodi ya 25% kwa uingizaji wa nywele zote bandia maarufu mawigi na 10% kwa zinazotengenezwa nchini katika jitihada za kukuza uchumi wa nchi. Waziri Philip Mpango ametangaza hatua hizo, ambazo zitaidhinishwa mwanzoni mwa mwezi ujao kama sehemu ya bajeti iliyosomwa jana, ya mwaka 2019 na 2020. Kadhalika kodi kwa visodo imerudishwa kutokana na kwamba hatua ya kuondoshwa kodi mwaka jana kwa bidhaa hizo muhimu kwa wanawake, haikusaidia kushuka kwa bei. Na badala yake Mpango ameeleza kuwa ni wafanya biashara wanaofaidi kutokana na kuondolewa kwa kodi hiyo. wanawake wengi huvaa nywele hizo bandia ambazo kwa wingi husafirishwa kutoka mataifa ya nje . Kwa makadirio, wigi hugharimu kati ya $4 na hata zaidi ya $130. Kwa nini wanawake wanakuza nywele zao mwezi Januari Meya awasuka nywele wanawake kuvutia kura Ghana Je mtindo wako wa ususi unamaliza nywele zako kichwani? Nchi ya Uganda, pia imeidhinisha kodi kwa mawigi, ndevu bandia, kope na nyusi za kubandika kwa 35%. Hii ina maana kwamba sekta ya urembo ambayo ni muhimu hususan kwa vijana na wanawake, itaathirika katika siku zijazo. Kodi mya pia inatarajiwa kuidhinishwa Uganda katika siku zijazo kwa vipodozi vinavyoingizwa nchini kukitarajiwa kukusanywa mapato ya hadi shilingi bilioni 11.6 za Uganda ,kutokana na kodi itakayotozwa kwa bidhaa hizo. Imepokewaje hatua hii? Wanawake wengi katika makundi ya WhatsApp na mitandao ya kijamii na hata wanaume wamekuwa wakizungumzia kuhusu pendekezo hilo: Wengine wakidhihaki namna baadhi ya wanawake waliozoea kutumia bidhaa hizo, sasa wanatatizika. Wengine wakitathmini athari kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wanaojishughulisha na uingizaji na utengenezaji wa nywele bandi. Annasatasia Sigera, mmiliki wa 'Wigs by Vianna' nchini Tanzania anasema ameshtushwa kusikia kutangazwa kwa kodi hiyo. ''Inaweza ikaathiri biashara, kwenye ongezeko la bei na hasaa kwa wauzaji wa ndani ya nchi ambao baadhi wana matawi yao nchini, wanaingiza kutoka China na kuzileta katika maghala yao'.. Anasema anaona kwamba huenda kukawa na shida mwanzoni, lakini mwisho wa kwisha anasema ni kwamba watu wanapenda nywele na watazidi kununua. Tofauti anaeleza ni kati ya watengenezaji na wanaonunua na kuingiza. ''Sisi ambao tunatengeneza tunajua namna gani ya kubana na kuifanya bei isipande sana, lakini kuna wanaonunua na kuuza kama zilivyo, hao ndio itakayowaathiri zaidi''. Kadhalika Ana, anasema huenda pia ikaathiri ubora wa nywele zinazoingizwa au kutengenezwa nchini. Kwasababu ya kupanda kwa bei, huenda wafanyabiashara wakaishia kununua nywele au wigi zisizo na ubora ili tu kupata faida ya kawaida na kuepuka kuingia hasara. Kwa upande mwingine Bi sigera anaeleza kwamba anaitazama hatua hii ya kuidhinishwa kodi kama fursa nzuri inayojitokeza katika kitengo au biashara ya nywele. Kwamba nywele zinamulikwa, Ana anasema utambulisho huo huenda unaashiria nafasi iliopo kwa wajasiriamali nchini. ''Lakini pia huenda ni fursa ya kuimarisha bidhaa zinazoingizwa nchini'' anasema Annasatsia. Kodi nyingine zilizopendekezwa Tanzania ni 35% kwa chokleti na biskuti ambazo awali zilikuwa zinatozwa 25%.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.