Marekani kufungua ubalozi mpya leo mjini Jerusalem


Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ofis ya ubalozi ambao itahudumu kama ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem
Marekani itafunguq ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa.
Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner.
Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria.
Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye.
Israel ilichukua udhibiti wa eneo la Jurusalem mashariki mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inahutaja mji huo kuwa wake na usiogawanwa
Hatua hiyo ya Trump ya mwaka uliopita ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilivunja msimamo wa wastani wa Marekani kwa suala la mji huo na kwenda kinyume na misimamo ya nchi zingine duniani.

Ni kipi kitafunguliwa na ni nani atahudhuria?

Ubalozi wa mdogo utaanza kutoa huduma kuanzia leo Jumatatu kwenye jengo la ofisi za ubalozi mjini Jerusalem.
Eneo lingine kubwa litatafutwa baadaye wakati ubalozi wote utahama kutoka mji wa Tel Aviv.
Sherehe za ufunguzi zilifanywa mapema ili ziweze kuenda sambamba na sherehe za miaka 70 za kuanzishwa taifa la Israel.
Rais Trump anatarajiwa kuhutubia wale ambaq watahudhuria sherehe hiyo kwa njia ya video.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ivanka Trump akimsalimia balozi wa Marekani nchini Israel David Friedman pamoja na mumewe Jared Kushner (kulia) baada ya kuwasili Israel
Kando na Ivanka Trump na Jared Kushner ambao wote ni washauri wakuu kwenye Ikulu ya White House, Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan watakuwa kwenye sherehe hiyo.
Muungano wa Ulaya umepinga vikali kuhamishwa kwa ubalzo huo na mabalozi wengine wa nchi za EU hawatahudhuria sherehe hiyo.
Hata hivyo wanadiplomasia kadhaa wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo waakilishi kutoka Hungary, Romania na Jamhuri ya Czech ambayo ilizuia taarifa ya pamoja ya EU kuhusu suala hilo.
Marais wa Guatemala na Paraguay pia nao wanatarajiwa kuhudhuria; nchi hizo zote mbili ziliamua kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem baada ya Trump kutoa tangazo hilo.

Israel na Palestina wanafanya nini?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Israel imekuwa ikisherehekea
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitoa wito kwa nchi zote kujiunga na Marekani na kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem.
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameutaja uamuzi wa Trump kama dafrao ya karne.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wapalestina wameandamana kupinga kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani
Maefu ya Wapalestina wanakusanyika kuandamana kwenye ua unaotenganisha Israwl na ukanda wa Gaza.
Muda wa kuhamishwa ubalozi huo umezua wasi wasi wa kongezeka msukosko huko Gaza
Tangu mwisho wa mwezi Machi zaidi ya wapalestina 40 wameuawa na wanajeshi wa Israel wakati wa maandamano ya mpakani.
Mku wa shriika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ameilaumu Isreal kwa kutumia nguvu nyingi.
Hali ya mji wa Jerusalem ndiyo chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina.
Tangu mwaka 1967 Israel ilijenga makao mengine kwa karibu wayahudi 200,000 huko Jerusalem mashariki. Makao hayo yanatajwa kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa, licha ya Israel kupinga hilo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.