Kauli Ya Abbas Kandoro Baada Ya Rais Magufuli Kukata Jina Lake na Kutomchagua Kuwa Mkuu wa Mkoa


Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe  Magufuli  alitoa orodha ya wakuu wapya wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Katika orodha hiyo Rais Magufuli , amewaacha wakuu kadhaa akiwamo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro.

Kipindi cha Sun Rise cha Radio Times Fm, kimefanya mahojiano na Kandoro asubuhi ya leo, ambapo amekiri kuachwa kwake na kuongeza kuwa tayari amefikia kikomo cha uongozi kwa maana umri wake haumruhusu kuendelea kutumikia nyadhifa hiyo.

“Unajua kuna watu wakituona wanajua kwamba bado tupo kwenye ujana, Ndugu mtangazaji mimi nina miaka 66 sasa hivi, tayari umri umenitupa mkono katika nafasi hii.

“Haijanishtua kwa sababu wakati tunapewa hii mikataba tuliambiwa kabisa ukomo wa mkuu wa Wilaya ni miaka 60 na Ukuu wa Mkoa ni miaka 66, hivyo nmetimiza umri wangu kisheria na napenda nimshukuru Mh Rais kwa hili” Alisema Abbas Kandoro.

Mpaka kustaafu kwake, Kandoro amehodhi nafasi ya ukuu wa Mikoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na Mbeya.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.