KUMEKUCHA CCM,MKAPA,MWINYI WAJITOSA "KUCHINJA" MAJINA YA WATAKA URAIS CCM,SOMA HAPO KUJUA

 




 
Zikiwa zimebaki siku 9 kabla ya kamati kuu ya chama mapinduzi CCM akijakutana kwa ajili ya “kufyeka” majina 37 kati ya 42 ya makada wake waliojitokeza na kuwania Urais ndani ya chama hicho,sasa jukumu lingine lawaangukia viongozi wastaafu wa chama hicho.
  Viongozi hao ambao ni marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa ambao wote kwa pamoja wataunda Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanya kikao wakati wowote wiki hii kujadili mwenendo wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho.
        Taarifa kutoka chanzo kimoja ndani ya CCM kimeeleza kuwa Mwinyi, Mkapa na wazee wengine wanaounda Baraza la Wazee la Ushauri, watapasua kichwa wiki hii kujadili mwenendo wa urais ikiwa ni siku chache kabla ya kufikia Julai 2, mwaka huu, inayoonyeshwa katika ratiba ya uchaguzi ya CCM kuwa ndiyo siku ya mwisho ya kurejesha fomu kwa wanaowania urais.
Lengo la kikao cha Wazee ni kujadili kwa kina mwenendo wa mchakato wa kumpata mgombea urais na mwishowe kutoa mapendekezo yao juu ya namna bora ya kumpata mgombea kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM (CC)
 
"Kikao hiki ni muhimu kwa hatma ya mchakato wa uchaguzi... baada ya kutofanyika wiki iliyopita, sasa kitafanyika wiki hii, tena wakati wowote kuanzia kesho (leo)," chanzo kilieleza.
    Mtoa taarifa huyo wa Mtandao huu ameongeza kwa kusema kuwa “hapa sikufichi wazee hawa wanaweza kuja na mapendekezo ambayo yatakuwa magumu kwenye wagombea ambao wamewai kukumbwa na kashfa ya Ufisadi,maana kunawagombea wametengeneza makundi makubwa kwenye chama chetu tena makubwa sana na Busara hizi za wazee zinaweza kuwaweka wagombe wenye Kashfa kubwa”amesema
   Makada hao wa CCM ambao wanawakati mgumu ni Waziri mkuu aliyejiuzelu kwenye Kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni tata ya kufua umme ya Richmound,Edward Lowassa pamoja na Waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye anathumumiwa kwa kitendo chake cha kufumbia macho uporaji wa Mabilioni ya Fedha kwenye Akaunt ya Tegeta Escrow.
         Awali, kikao hicho kilitarajiwa kufanyika Jumatano iliyopita jijini Dar es Salaam lakini kikaahirishwa na Katibu wa Baraza la Ushauri la Wazee, Pius Msekwa, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni baadhi ya viongozi wakuu wa CCM kuwa safarini.
 
Alipoulizwa  na chanzo changu jana iwapo watakutana kaunzia leo, Msekwa hakuwa tayari kueleza kiundani na badala yake alimjibu mwandishi kwa kifupi: "Just pay attention (wee jiweke tayari tu) kama umesikia juu ya kikao chetu."
        Kikao cha Baraza la Ushauri la Wazee ni mahususi kwa ajili ya ushauri juu ya watia nia 42 wa urais waliojitokeza kutaka kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera yake katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Wanaounda baraza la wazee
          Wanaounda Baraza la Ushauri la Wazee kwa mujibu wa mabadiliko yaliyofanywa na CCM mwaka 2012 katika katiba yake ni marais wastaafu Mwinyi (Mwenyekiti), Mkapa (Mjumbe), Amani Abeid Karume (Mjumbe) na Dk. Salmin Amour (Mjumbe).
         Wengine ni Waziri Mkuu mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais, John Malecela (mjumbe) na Pius Msekwa (Katibu).
 
         Mkutano huo wa Baraza la Wazee CCM ni utangulizi wa mfululizo wa vikao vingine vya chama hicho vitakavyoanza Julai 5, mwaka huu.
            Vikao vingine ambavyo viko katika maandalizi ya kukutana ni Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa itakayokutana Julai 7 na Kamati Kuu (CC) itakayokutana Julai 8, chini ya Rais Kikwete, ikifuatiwa na kikao cha NEC Julai 9, mwaka huu.
            Jina la mgombea urais atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu litajulikana Julai 12 baada ya kupigiwa kura na Mkutano Mkuu wa          Taifa wa CCM, ambao ni maalum kwa ajili kuchagua jina la mgombea mmoja kati ya watatu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.