Wizara Zinazotarajia Kufutwa na Magufuli Hadharani.......
Chanzo kimoja kutoka serikalini kimeiambia Nipashe jana kuwa wizara hizo zitaunganishwa kwenye wizara mpya zitakazoanzishwa na Rais ambaye ameweka mkakati wa kuwa na baraza dogo la mawaziri.
Wizara zinazotajwa kufyekwa ni Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Wizara Ofisi ya Waziri Mkuu na Sera, Uratibu na Bunge.
Nyingine ni Wizara Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Wizara ya Nchi, Ofisi Makamu wa Rais Mazingira na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Kadhalika, katika mabadiliko hayo, wizara nyingine zitaguswa ili kufikia malengo ya kubakia na wizara chache kutimiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kubana matumizi na kuinua maisha ya Watanzania.
Chanzo hicho kimebainisha kuwa Rais Dk. Magufuli atalitangaza Baraza la Mawaziri ndani ya wiki hii ingawa bado kumekuwa na usiri wa siku halisi atakayotangaza.
Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, ilimaliza muda wake Novemba 5, mwaka huu ikiwa na wizara 30. Vile vile, alipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 2005, Rais Kikwete alikuwa na serikali kubwa yenye mawaziri na naibu wao zaidi ya 60.
Rais Magufuli aliyeapishwa Novemba 5, mwaka huu, tayari ameshamteua Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa serikali yake na Ijumaa iliyopita alizindua rasmi Bunge la 11.
Juzi, chanzo kimoja kililiambia Nipashe kuwa tayari Rais Magufuli kwa kushirikiana na wasaidizi wake, ameshakamilisha sehemu kubwa ya mchakato wa kuunda baraza lake la mawaziri na kwamba kinachosubiriwa sasa ni kulitangaza wakati wowote kuanzia sasa
Maoni
Chapisha Maoni