Mugabe: Raila Odinga Akikanyaga Zimbabwe Nitamkamata Na ‘Kumhasi’
Akizungumza huko Marondela katika hafla iliyowahusisha wanajeshi
walioshiriki katika vita mbalimbali, Mugabe alimtuhumu Raila kwa kutaka
kumpindua kwenye nafasi yake kwa kuwapandikiza wapinzani nchini humo.
Hivi ndivyo alivyosema:
“Raila Odinga ni mwanasiasa muongo wa Kenya, mwanaume mnafiki ambaye
yuko katika mkakati wa kuwapandikiza marafiki zake kuwa marais kwenye
nchi zote za Afrika ili awe mwenyekiti mwenye nguvu kwenye Umoja wa
Afrika (AU), siku moja watamuangusha kwenye sanduku la kura.
“Angalia alichokifanya Nigeria, Tanzania, Ivory Coast na anataka kufanya
hivyo pia Uganda kwa kumtumia rafiki yake Kiiza Besigye ambaye leo
anapewa sifa na ushupavu ambao anapata kutokana tu na amri za Raila
barani Afrika.
“Hapa hatutamruhusu kuwageuza marafiki zake wa zamani Tendai Biti na
Morgan kuniondoa mimi, hakuna kwa namna yoyote. Nitatawala kwa miaka 90
zaidi. Nimekiamuru kikosi maalum cha jeshi kuangusha ndege yoyote
itakayokuwa imembeba huyo mwendawazimu Raila na kundi lake la mipango ya
uchakachuaji wa kura dhidi ya marais wanaoendelea kutawala Afrika.
“Nimewaamuru walinzi wangu kuhakikisha wanakuwa makini kuhakikisha Raila hajipenyezi bila kubainika.
“Tutashindwaje kukosa usingizi kwa sababu tu ya Raila, yeye ni kitu
gani? Tutamkamata na kumhasi kabla yeye na timu yake hawajamsaidia
Morgan na Biti kunipindua kwenye Urais.”
Hii sio mara ya kwanza kwa Mugabe kushambulia Kenya kwa maneno, wiki
chache zilizopita alidai kuwa wananchi wa Kenya ni wezi kutoka damuni na
kwamba anadhani wanasomea shahada ya wizi. Alitahadharisha wananchi
wake kutokubali kukaa karibu na wakenya kwa madai kuwa wanaweza
kuwaambukiza wizi.
Maoni
Chapisha Maoni