MWIGULU LAMECK NCHEMBA AZUA GUMZO KUBWA WAKATI AKIAPA BUNGENI TAZAMA HAPA LIVE
Mwigulu Lameck Nchemba Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi akiapa mbele ya Spika Job Ndugai.
Mwigulu
Lameck Nchemba Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi amezua gumzo Bungeni
katika kikao cha Bunge la 11 kilichoketi leo asubuhi wakati Spika wa
Bunge Bw.Job Ndugai akiwaapisha wabunge wateule kuwa wabunge rasmi.
Katika
zoezi hilo la kuapa ambapo wabunge mbalimbali wamelipitia,kila Mbunge
anafika mbele ya Spika na kupewa kitabu chenye maelezo ya kuapia ambapo
wabunge asilimia kubwa wamekuwa wakisoma ila ilipofika zamu ya Nchemba
imekuwa tofauti ambapo yeye hakukifungua kitabu chenye maelezo ya
kuapaia na badala yake kuapa pasipo kusoma kitabuni.
Mara
baada ya kumaliza kuapa wabunge walisikika wakimshangilia kwa kumpigia
makofi huku baadhi yao wakisema kuwa ‘amekariri’.“Du,amekariri hadi
maneno ya kuapia kweli jamaa kiboko” alisikikika akisema mmoja wa
wabunge bungeni hapo.
Mara
baada ya kuapa Nchemba anakuwa sasa ni mbunge rasmi ambapo anaweza
kuanza kutekeleza majukumu kama mbunge halali wa jimbo la Iramba
Magharibi.
Maoni
Chapisha Maoni