CHADEMA Washinda Kesi ya Pingamizi la Polisi, Sasa kesi ya Msingi kusikilizwa

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Lameck Mlacha, ametupilia mbali mapingamizi yaliowekwa na RPC wa Mwanza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa mleta maombi ambae ni Baba mdogo wa Mawazo hana uhalali wa kisheria wa kuleta maombi hayo kwa kuwa yeye si baba mzazi wa marehemu, na kuwa hajaleta hoja za kubishaniwa kwenye maombi hayo. Upande wa utetezi unaoongozwa na mawakili John Mallya, James Millya na Paul Kipeja ulijibu hoja hizo kuwa katika hatua hiyo masuala ya kubishaniwa hayana sababu ya kuletwa kwa kuwa ni hatua ya awali sana.

Kuhusu uhalali wa kisheria wa baba mdogo wa marehemu, majibu yalikuwa kwamba baba mdogo kwa kuwa ndiye aliemlea Marehemu Mawazo, anayo mamlaka na uhalali wa kisheria wa kuleta maombi hayo.

Mahakama imekubaliana na hoja za mawakili wa mleta maombi na kuamua kuruhusu kesi ya msingi kufunguliwa kama ilivyoombwa, na kutupilia mbali mapingamizi ya RPC na AG.

Upande wa wapeleka maombi utawasilisha maombi ya kesi ya msingi leo hii mchana, kisha tutasubiri maelekezo ya Mahakama kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa lini kisha uamuzi wa kesi hiyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA