MADAI MAZITO: MKONGWE LADY JAY DEE KWISHA JEURI YAKE


Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’MAISHA bwana! Kuna madai kwamba, nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ambaye ni ‘mtalaka’ wa Mtangazaji Gardner G. Habashi ‘Kapteni’ kwa sasa si kama yule wa zamani akisemekana kuishiwa ‘mpunga’ kiasi cha mambo yake kwenda halijojo lakini kisa kikuu kikitajwa ni kitendo cha ndoa yao kuparanganyika.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Jide kwa sasa hana zile mbwembwe zake za kuonekana mjini akitanua na gari la kifahari kwenye maeneo mbalimbali ya kujidai kwa vile miradi yake mingi imefunga breki.
MGAHAWA, BENDI VYATAJWA 
“Ninachowaambia ni kweli kabisa jamani! Jide wa sasa si yule wa enzi zile. Nikishibisha maneno yangu, Jide ameshindwa kuuendeleza Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Kinondoni mpaka ukafulia, hilo mnalijua na kwa sasa mgahawa unamilikiwa na mfanyabiashara mwingine na ameupa jina lingine. 

“Lakini ukiachana na mgahawa, wewe jiulize, mara ya mwisho kuisikia bendi ya Jide ya Machozi ikiwa jukwaani ni lini? Pia bendi imesimama! Yaani mambo yake hayaendi sawasawa kama awali,” kilisema chanzo hicho. 

GARDNER KACHANGIA? 
Chanzo hicho kiliendelea kuweka wazi kuwa, baadhi ya marafiki wa zamani wa familia ya Jide na Gardner wamekuwa wakidai kwamba, kitendo cha wawili hao kutengana kiliondoa sehemu kubwa ya nguvu iliyokuwa ikisaidia kwenye biashara. 

“Unajua Gardner licha ya kuwa mumewe, lakini pia alikuwa meneja wake. Ndiye aliyekuwa akisimamia Bendi ya Machozi na pia alikuwa akisimamia mradi ule wa mgahawa. Si unajua kwa mambo kama haya, mchango wa Gardner ulikuwa mkubwa. 
“Sasa kuachana kwao, automatiki Gardner akawa si meneja wa Jide tena, matokeo yake Jide akashindwa kusimamia miradi yake mwenyewe, ndiyo haya unayoyaona sasa,” kilisema chanzo. 

ATHARI ZA GARDNER ZIMEJIFICHA 
Kwa upande wake, Gardner anatajwa kuendelea na maisha yake vizuri kwani mpaka sasa ni Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha E FM cha jijini Dar akionekana kutopigika sana na athari za kutengana kwao. 

JIDE ALIVYOTAFUTWA
Risasi Jumatano lilimsaka Jide kwa nguvu zake zote ili kumpa nafasi ya kufafanua madai hayo lakini kwa simu yake ya mkononi hakuwa hewani. 
Risasi Jumatano lilifunga safari mpaka kwenye makazi anayodaiwa kuishi hivi sasa maeneo ya Masaki, Dar lakini nyumba hiyo ilionekana kuwa kimya sana. 

Baadhi ya majirani walisema hawajamuona kwa siku kadhaa sasa huku wengine wakisema wanaamini amesafiri nje ya nchi. 
“Mh! Jideee… Jideee! Kwa kweli sijui kama yupo hapa nchini. Inawezekana yupo lakini pia inawezekana hayupo. Mi binafsi sijamwona siku nyingi,” alisema jirani mmoja bila kujitambulisha jina. 

GARDNER AOMBA UDHURU 
Kwa upande wake, Gardner alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu madai hayo aliomba udhuru wa dakika kadhaa akisema atapiga yeye ingawa hakufanya hivyo. 

Kumbukumbu zinaonesha kuwa, mara zote ambazo Gardner amekuwa akipigiwa simu na waandishi wetu na kuombwa kufafanua kuhusu tuhuma kadhaa, amekuwa akijibu atapiga yeye baadaye au kusema hana la kuchangia!! 

MTABIRI ATIA NENO ZITO 
Hata hivyo, katika moja ya elimu zake za nyota, mtabiri maarufu nchini ambaye pia ni mtoto wa aliyekuwa mnajimu maarufu Afrika Mashariki, marehemu Shehe Yahya Hussein, Maalim Hassan alipoulizwa kuhusu maendeleo ya Jide alisema kuwa, kufifia kwake kunatokana na kutembelea nyota ya Gardner. 
“Yule alikuwa juu kwa sababu alikuwa akitembelea nyota ya yule aliyekuwa mume wake. Sasa kwa kuwa waliachana, lazima afifie kwa vile nyota ya yule ilikuwa kali kuliko yeye,” alisema Maalim Hassan katika mahojiano maalum nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA