HATIMA YA MWILI WA MAREHEMU MAWAZO KUAGWA JIJINI MWANZA KUAMULIWA KESHO NA MAHAKAMA.
Mwenyekiti
wa Chadema Freeman Mbowe akitoa taarifa kwa wananchi baada ya Chadema
Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili
wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema leo kimefungua kesi katika Mahakama
Kuu Kanda ya Mwanza, ili kuiomba Mahakama hiyo kutengua zuio la kuuaga
mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita Marehemu
Alphonce Mawazo, lililotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kutokana
na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu.
Katika
kesi hiyo, Chadema inawakilishwa na Mawakili watatu ambao ni James
Millya, John Mallya pamoja na Paul Kipeja ambapo mlalamikaji ni Charles
Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo.
Mahamaka
hiyo chini ya Jaji Lameck Mlacha, imesikiliza malalamiko ya upande wa
washtaki na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo imeamuru mlalamikiwa
ambae ni Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza pamoja na mwanasheria Mkuu wa
Serikali kupelekewa nyaraka za kesi hiyo kabla ya kusikiliza utetezi wao
hapo kesho.
Mapema
kabla ya kesi hiyo kusikilizwa, wafuasi wa Chadema waliokuwa
wamekusanyika nje ya viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza,
walilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani hapo
ili kujua hatima ya kesi hiyo, ambapo wamesema kitendo hicho kinaondoa
dhana ya Rais John Pombe Magufuli, kuwa yeye ni rais wa wananchi wote
wakati wao kama Chadema wananyimwa haki zao.
Licha
ya Malalamiko hayo pamoja na ulinzi mkali wa polisi uliokuwa umetanda
Mahakamani hapo, bado wafuasi wa Chadema hawakuondoka katika viunga vya
Mahakama hiyo hadi pale Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe
alipowasihi kurejea majumbani mwao hadi kesho kesi hiyo itakaposikilizwa
tena.
Ni
zaidi ya siku nane sasa tangu marehemu Alphonce Mawazo auawe kikatili
Mkoani Geita na watu wasiojulikana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa
ni chuki za kisiasa ambapo mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya
Rufaa ya Bugando.
Mmoja
wa Mawakili wa Chadema John Mallya akitoa taarifa kesi baada ya Chadema
Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili
wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.
Kesi
ilisikilizwa katika Jengo la Mahakama ya Biashara lililopo katikati ya
Jiji la Mwanza. Pichani ni mawakili wa Chadema wakielekea mahakamani
huku kukiwa na umati wa wafuasi wa Chadema (Ukawa) pamoja na viongozi
waandamizi wa Chadema

wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia
kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na
Chadema hii leo

Chadema hii leo.
Maoni
Chapisha Maoni