HAWA NDO WABUNGE 15 WAREMBO ZAIDI KATIKA BUNGE HILI JIPYA
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Sifael Paul na Brighton Masalu
Upande
wa pili! Bunge la 11 liliahirishwa Ijumaa iliyopita ambapo Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliwahutubia
wabunge huku Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akihitimisha hotuba
kwa kuliahirisha rasmi bunge hilo hadi Januari 26, mwakani.
Hata hivyo, hiyo siyo hoja
wala gumzo kuu la bunge hilo ambalo linajumuisha wabunge wengi wapya
kutoka vyama mbalimbali, lakini ‘pointi’ kubwa ni jinsi wabunge 15
wanawake ambao walilitikisa bunge hilo kutokana na urembo wao na kuzua
gumzo kubwa.
Wabunge hao warembo a.k.a
visu ambao umri wao bado ni ‘asubuhi’, walikuwa kivutio machoni mwa
baadhi ya wabunge hususan vijana ambao ‘walivunjika’ shingo juu ya
wawakilishi hao.
Ijumaa Wikienda linakupa
orodha ya wabunge hao warembo ambapo waliojulikana kwa kukimbiza kama
akina Halima Mdee wametakiwa kukaa chonjo. Hata hivyo, wabunge warembo
wa kike ni wengi, lakini wafuatao ndiyo ‘shida’ kuanzia maumbo na sura
zao.
CATHERINE MAGIGE (CCM)
Rekodi ya urembo wake
haijawahi kuvunjwa bungeni. Mara zote, tangu alipotinga bungeni mwaka
2010, amekuwa gumzo kubwa kwa uzuri wake, licha ya kushindanishwa na
wabunge kadhaa, lakini bado ‘anatusua’ vilivyo.
BONNAH KALUWA (CCM)
Hii ni mara yake ya kwanza
kuingia bungeni. Uzuri na urembo wake umeonekana gumzo bungeni tangu
mwanzo hadi mwisho wa kikao hicho. Sura, umbo na macho yake vimekuwa
kivutio kikubwa.
ANGELLA KAIRUKI (CCM)
Ukimwangalia vibaya,
unaweza kusema ni shombeshombe. Urembo wa sura yake, umekuwa ukiwapa
nyakati ngumu watu wengi, wakati mwingine kushindwa hata kung’amua kama
ana asili ya Kiarabu au la! Kinachomuongezea sifa katika kilinge cha
urembo ni umbo lake lililojengeka.
ESTER MATIKO (CHADEMA)
Achana na ukali wa hoja
zake anapochangia mijadala. Hiki ni ‘kisu’ kikali kinachovutia bungeni.
Umbo lake la ‘kitoto’, uzuri wa sura na macho ya mviringo, vinamfanya
aonekane mrembo na mwenye uzuri wa kupindukia.
LOLESIA BUKWIMBA (CCM)
Tabasamu lake ndiyo
limekuwa gumzo. Sura yenye uchangamfu imekuwa ikiteka macho ya watu
wengi. Kamwe huwezi kuchoka kumtazama mwakilishi huyo. Mpole kama
alivyo, lakini amekuwa ‘akikimbiza’ vilivyo mjengoni.
DK MARRY MWANJELWA (CCM)
Licha ya umri kuanza
kumpigia honi lakini anawafunika wabunge wengi wenye umri mdogo. Urefu
na figa nzuri, vinachangia kwa kiasi kikubwa kumweka kwenye orodha ya
wabunge wa kike wanaotikisa kwa uzuri.
UMMY MWALIMU (CCM)
Hana makuu. Mpole na mwenye
aibu wakati wote, lakini urembo wake unashereheshwa na umbo lake
matata. Ana urembo wa haja unaoyapa macho kazi ya ziada kuitafuta kasoro
yake.
CECILIA PARESSO (CHADEMA)
Urembo, uzuri wa umbo lake, urefu, unene wa wastani na sura nzuri vinatosha kumuingiza kwenye orodha hii.
JULIANA SHONZA (CCM)
Umbo lake ni la kawaida, lakini shughuli iko usoni. Achana na sehemu zingine za mwili, ukimtazama usoni tu utagundua ni kisu.
LUCY MAYENGA (CCM)
Ni mrembo wa umbo na sura.
Hahitaji maneno mengi kumwelezea, lakini ukweli unabaki palepale kuwa ni
miongoni mwa wabunge warembo walioupa shida Mji wa Dodoma.
MBONI MHITA (CCM)
Akiwa umbali kidogo kutoka
mahali ulipo, unaweza kumchukulia kawaida! Shughuli ipo akikusogelea.
Umbo na uzuri wake ni habari nyingine.
NEEMA MGAYA (CCM)
Rangi yake ya asili, ngozi
laini, umbo namba nane na ucheshi wake, vinamtetea kuingia kwenye ulingo
wa wabunge hawa warembo zaidi.
VICKY KAMATA (CCM)
Silaha kubwa aliyonayo ni
midomo na macho! Geuza gazeti nyuma, mtazame tena Vicky, unaona? Si
umbo, si sura, si macho, si mdomo, Vicky Kamata ni mrembo. Inatosha
kusema hivyo tu.
JESCA KISHOA (CHADEMA)
Ni mrembo anayevutia kwenye
viunga vya bungeni na inawezekana ndiyo maana aliyekuwa Mbunge wa
NCCR-Mageuzi, David Kafulila aliamua kuchukua jumla na kumweka ndani.
ESTER BULAYA (CHADEMA)
Kama unahitaji kumpongeza
muumba kwa kazi njema, wewe mtazame Ester Bulaya, si mrefu, si mfupi, si
mweusi wala si mweupe. Yuko kati kwa kati. Akitembea, kama ni
barabarani, jihadhari na vyombo vingine vya usafiri.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni