Safari ya Miss Tanzania kusogelea headlines za fainali za Miss World 2015 imesogea hatua moja mbele ambapo mrembo wetu, Lilian Deus Kamazima tayari katua China kuungana na warembo wengine zaidi ya 100 toka nchi mbalimbali kushiriki kwenye fainali yenyewe.
Kama hujajua basi naomba nikuweke karibu na ratiba yenyewe mtu wangu, ni kwamba Lilian aliondoka TZ November 19 2015 kuelekea Sanya China ambapo watakaa kambi kwa muda wa kama wiki nne hivi.
Fainali ya Miss World itakuwa December 19 2015 hukohuko Sanya China, hapa nimezipata pichaz za warembo wote 20 wanaowakilisha nchi mbalimbali za Afrika kwenye fainali za Miss World 2015.
Lilian Kamazima, mwakilishi wetu Tanzania kwenye Miss World 2015. (Umri- 19)
Mrembo kutoka Botswana, anaitwa Seneo Bambino Mabangano (Umri- 19)
Anaitwa Andrea N’Guessan Kakou, mrembo kutoka Ivory Coast (Umri- 23)
Jina lake ni Kisanet Teklehaimanot, mrembo kutoka Ethiopia (Umri- 21)
Anaitwa Reine Ngotala Obiang, umri wake ni miaka 18, ni mrembo anayewakilishaGabon.
Mrembo wa Guinea, jina lake ni Mama Aissata Diallo (Umri 19)
Mrembo mwingine kutoka Guinea-Bissau, anaitwa Laila Elewar Da Costa (Umri- 18)
Jessica Ngoua Nseme, yeye ni mwakilishi wa Cameroon kwenye Miss World 2015. (Umri- 25)
Mrembo wa Kenya, anaitwa Charity Njeri Mwangi.. (Umri- 23)
Huyu anatoka Lesotho, anaitwa Relebohile Mamaphathe Kobeli.. (Umri- 19)
Mrembo wa Mauritius, Aureilla Begue… (Umri- 21)
Kutoka Namibia, huyu ni Steffi Van Wyk.. (Umri- 24)
Mrembo mwenye umri wa miaka 21 kutoka Nigeria, anaitwa Unoaku Anyadike
Linne Freminot kutoka Seychelles.. (Umri- 22)
Mrembo wa South Africa, Liesl Laurie (Umri- 24)
Ajah Deng kutoka South Sudan (Umri- 22)
Miss Uganda, Zahara Nakiyaga (Umri- 23)
Miss Zambia, Michelo Malambo (Umri- 24)
Mrembo anayewakilisha Zimbabwe, Annie-Grace Farayi Mutambu (Umri- 19)
Mwaka
2014 mrembo wa South Africa, aliibuka na ushindi wa Miss World, 2015
je? Yupi kakuvutia kati ya hao mtu wangu na unaona anafaa kuvaa Taji
hilo?
Rolene Strauss, Miss World 2014
Maoni
Chapisha Maoni