BREAKING NEWS! MH. KASSIM MAJALIWA NDIYE WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Hatimaye kitendawili kimeteguliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli
baada ya kumteua Mh. Kassim Majaliwa Mbunge wa Ruangwa mkoa wa Lindi na
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi anayeshughulia elimu kuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitangaza jina hilo Spika wa
Bunge Mh. Job Ndugai amewaeleza wabunge kuwa kwa mujibu wa katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa rais kuteua jina la Waziri Mkuu
na kuliwasilisha bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na wabunge
Hivyo bunge litamthibitisha rasmi
na kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Fullshangwe na
kikosi chake chote kimatakia Mh. Waziri Mkuu Mteule Kassim Majaliwa
afya njema na mafanikio katika majukumu yake mapya.
Maoni
Chapisha Maoni