MANENO 34 YA MKE WA RAIS MUGABE WANAOVAA SKETI FUI NA SURUALI ZA KUBANA
Huu ujumbe umetoka kwa mke wa Rais wa Zimbabwe, Mama Grace Mugabe na
umetolewa kwenda kwa warembo wote wanaopendelea vimini na suruali za
kubana, anasema lolote baya likikukuta basi ujue umejitakia !!
Kama na wewe uko kwenye list ya wanaopendelea kuvaa hivyo, basi maneno ya Mama Mugabe yakufikie >>> “Kama
unatembea huku umevaa kimini umeacha mapaja yako wazi, unawashawishi
wanaume wakutamani.. hapo kama ikitokea umebakwa utalaumu? Huo ni ujinga
wako mwenyewe.”– Mama Grace Mugabe.
Mama Grace Mugabe hakuishia hapo, ushauri wake ni huu hapa “Mnapaswa kuvaa kama mimi au kama unavaa suruali isiwe ya kukubana sana…“
Ujumbe wake unapingana na madai ya kikundi cha Katswe Sisterhood, kilichopo Harare Zimbabwe ambao wamewahi kuandamana wakitaka wanawake kuruhusiwa kuwa na uhuru wa kujichagulia mavazi ya kuvaa
Maoni
Chapisha Maoni