ZITTO KABWE ACHAFUA HALI YA HEWA ZANZIBAR,APEWA SIKU 14 KUOMBA RADHI LASIVYO KUPANDISHWA KIZIMBANI
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amepewa siku 14 kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa kumhusisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na makosa ya uhaini. Msimamo huo ulitolewa na wagombea wawili wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Juma Ali Khatib (Tadea) na Soud Said Soud, walipokuwa wakizungumzia kauli ya Zitto kudai haikuwa sahihi kwa Rais wa Zanzibar kubakia madarakani wakati serikali yake imefikia ukomo wake Novemba 2, mwaka huu. Soud alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Kifungu cha 28 (1)(a), Rais Shein ni Rais halali wa Zanzibar na atabakia madarakani hadi atakapochaguliwa rais mpya kwenye uchaguzi wa marudio. Alisema kuwa Dk. Shein alichaguliwa na wananchi wa Zanzibar na haikuwa haki kwa Zitto kumhusisha na makosa ya uhaini kwa kuendelea kubaki madarakani kwani yuko kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. "Zitto Kabwe afute kauli yake na kuwaomba radhi wananchi wa Zanzibar ndani ya siku 14 na...