WEMA ASHTAKIWA KWA KOVA


Waandishi wetu

KIMENUKA! Mtangazaji na MC (master of ceremony) maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ ameivalia njuga tabia ya mastaa kuhusika na matusi ya mtandaoni na kupiga picha za utupu ambapo kwa kuanza amemshitaki mwanadada Wema Isaac Sepetu kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova akimtuhumu kuwa kati yao.
Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu.
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum huku akirekodiwa ili kuweka kumbukumbu vizuri, Mai alisema yeye ni mmoja wa wahanga wa matusi ya mtandaoni…
Waandishi wetu
KIMENUKA! Mtangazaji na MC (master of ceremony) maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ ameivalia njuga tabia ya mastaa kuhusika na matusi ya mtandaoni na kupiga picha za utupu ambapo kwa kuanza amemshitaki mwanadada Wema Isaac Sepetu kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova akimtuhumu kuwa kati yao.
Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu.
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum huku akirekodiwa ili kuweka kumbukumbu vizuri, Mai alisema yeye ni mmoja wa wahanga wa matusi ya mtandaoni na amegundua wanaomtukana ni kundi linalojiita Team Wema.
Msikie Mai
“Kuna watu kwenye hii mitandao ya kijamii wamejipa majina bandia lakini ukiwafuatilia sana utagundua ni watu wa Wema, ni watu ambao ukimtibua Wema watakuvaa kwa kukutukana sana.
“Hao hao ndiyo wanaoongoza kwa kumsifia sana Wema kwenye mitandao. Ili ujue kwamba Wema anawajua, huwa wanampelekea hadi zawadi na juzijuzi hapa walihamasishana kuchanga fedha ili wampelekee Wema.
Mtangazaji na MC (master of ceremony) maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’.
“Sasa kama ni watu anaowajua, kwa nini asiwazuie kutukana ovyo watu? Tutakuwa tunakosea kusema anawatuma?
“Hebu fikiria Wema anataka kugombea ubunge, hilo ni jambo jema na sisi wenzake tunamuunga mkono lakini nafasi hiyo ataimudu kweli kama anashindwa ‘kuwakontroo’ watu walio nyuma yake ambao wanawakosesha amani wenzao?
“Kitu ambacho nakiamini ni kwamba, usimuone Wema kakaa kimya kwenye akaunti yake lakini hawa mastaa unaowaona wanatukanwa, baadhi ya watukanaji wanatumwa na Wema, wanaambiwa fulani tukana, fulani tukana,” alidai Mai.
Wema anahusikaje?
Kwa madai yake, Wema anahusika kwenye kushamiri kwa tabia hii kwa kuwa, watu wake ndiyo wamekuwa wakisumbua na dalili za wazi zinaonesha ‘anawa-push’ kiaina kufanya hivyo.
Awagusa Diamond, Kajala, Aunt
“Mara kadhaa tumekuwa tukiona Wema akiwaambia Team Wema wasimtukane Diamond (Nasibu Abdul), tunaona mastaa wakitofautiana na Wema kidogo wanashambuliwa kwa matusi, mfano Kajala (Masanja) na Aunt (Ezekiel).
“Wanaofanya hivyo siyo mashabiki wa Wema, ni marafiki wake damdam na ni jambo ambalo Wema analijua, ndiyo maana anaweza kuwaambia wasimtukane f’lani.
“Kwa nini asiwazuie waache tabia ya matusi mtandaoni ambayo ni kinyume na sheria?” alihoji Mai.

Kajala Masanja.
Agusia picha chafu
Katika kufunguka kwake, Mai alienda mbele zaidi kwa kumtaka Wema kujiangalia upya ikiwa ni pamoja na kuwakontroo marafiki zake wasitukane watu lakini pia aache kupiga picha za utupu, alizopiga huko nyuma zinatosha, ajitahidi kuwa msafi.
Ashitakiwa kwa Kova
Huku akionekana kuwa makini sana na kutaka taarifa anazotoa zilifikie jeshi la polisi na kuzifanyia kazi, Maimartha aliamua kumshitaki Wema moja kwa moja kwa Kamanda Kova akimtaka achukue hatua stahili ili kukomesha tabia hiyo.
“Sasa naomba leo niseme kwamba, mtandaoni hatutaki matusi na doria zipo, wapo wana usalama, mimi nakuambia Kamanda Kova, hili nalifikisha kwako nikijua jeshi lako linahusika.
“Mitandaoni watu wamechoka kutukanwa, naomba hizo doria zifanye kazi na kama utataka ushirikiano, mimi nipo na nitatoa ushahidi ukitaka.
Wema anasemaje?
Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Wema ili kuzungumzia tuhuma hizo lakini simu yake iliita bila majibu na hata alipotumiwa meseji hakujibu.
Aidha, wanahabari wetu walifunga safari hadi nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar lakini waliishia getini baada ya kuambiwa hayupo. Jitihada za kumtafuta zinaendelea ili naye afunguke.
Ofisini kwa Kova
Kutokana na mashitaka hayo ambayo Mai alitaka yamfikie Kamanda Kova, waandishi wetu walimtafuta ‘afande’ huyo lakini jitihada hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Kamanda Suleiman Kova.
Hata hivyo, mmoja wa maafisa wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar aliyeomba hifadhi ya jina alisema, kama Mai ana madai yake hayo anatakiwa ayawasilishe kwa Kova ‘fizikale’ na kama ataridhika naye, atayachukua na kuyapeleka kwa ofisa upelelezi wa kanda ‘Zonal Crime Officer’ ambaye atayafanyia kazi bila kujali majina ya wahusika.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA