LULU AZUIWA KUMSHIKA MKONO MAMA SALMA KIKWETE

 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete (Picha na Mtandao).
Ilikuwaje? Taarifa ikufikie kuwa, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael `Lulu’ aliibua minong’ono kwenye msiba wa mwanamuziki Ramadhan Masanja `Banza Stone’ baada ya kutaka kumsalimia kwa kumshika mkono mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael `Lulu’.
Chanzo chetu kilichoshuhudia tukio hilo lililojiri hivi karibuni kilisema kuwa Lulu aliingia nyumbani kwa wazazi wa Banza, Sinza-Lion, Dar ili kuwasalimu wafiwa lakini baada ya kumuona Mama Salma Kikwete alijisogeza jirani kwa lengo la kutaka kumsabahi lakini walinzi wake walimzuia kwa kuwa ni kinyume na utaratibu.
Baada ya kubwagiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Lulu ambapo awali alidai hakumuona msibani hapo, lakini baadaye alikiri kumuona ila hakupata fursa ya kumsalimia naye.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA