DODOMA KIMENUKA ONA SASA YALIYOKWISHAJIRI HOSPITALI ZATAYARISHWA KUHUDUMIA MAJERUHI WA MATOKEO
MAJINA MATANO NGOMA NZITO: Mizengwe yatawala hadi usiku wa manane Kamati Kuu kufyeka waliodaiwa kuanza kampeni mapema.
Kamati
Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imejikuta ikiwa katika kibarua kizito
cha kuteua watia nia watano kati ya 38 wa nafasi ya urais mjini Dodoma
jana usiku baada ya kuwapo kwa msuguano mkali juu ya watu wa kuwaondoa
kwa tuhuma za kuanza kampeni mapema.
Taarifa
kutoka chanzo kimoja cha uhakika ndani ya CCM kilieleza kwamba kulikuwa
na mizengwe ya kuwapo kwa barua kutoka kwa vigogo wenye ushawishi mkubwa
ndani ya chama hicho kushinikiza kuondolewa kwa baadhi ya wagombea kwa
madai kuwa walianza kampeni mapema na hivyo kuhatarisha hatma ya
ushiriki wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25,
mwaka huu.
Hali hiyo
inaelezwa kwamba ndiyo kigezo ambacho wajumbe wa Kamati Kuu waliokutana
kwenye ofisi moja nyeti mjini Dodoma waliendelea kuishikilia kwa lengo
la kuwaondoa wagombea wenye dosari hizo.
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya wajumbe walikuwa kwenye mjadala mkali
kutokana na hofu kuwa wakiteuliwa watia nia walioanza kampeni mapema
watakiweka chama chao katika hatari ya kuwa na mgombea aliyepoteza sifa
kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi mkuu zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi.
Hadi
kufikia mishale ya saa 7:31 usiku hakukuwa na taarifa zozote za matokeo
ya majina matano yaliyopitishwa na Kamati Kuu kati ya 38 ya waliorejesha
fomu ili yapelekwe kwenye kikao cha Nec kwa mchujo zaidi ili wabaki
wanafainali watatu.
USIRI MKUBWA WATAWALA
Kama
ilivyotarajiwa, kikao hicho cha Kamati Kuu, kilifanyika kwa usiri mkubwa
kiasi cha kuwafanya waandishi wa habari kuwa na wakati mgumu kupata
taarifa zilizokuwa zikiendelea ndani yake.
Awali
kabla ya Kamati Kuu ya chama hicho kukutana kwa kazi hiyo, siri nzito
ilitenda juu ya maamuzi yaliyofanywa na kikao cha Kamati ya Usalama na
Maadili ya CCM kilichoketi juzi usiku chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,
Rais Kikwete. Kikao hicho cha Kamati ya Usalama na Maadili ya CCM,
kilikaa kupitia mafaili ya wagombea 38, waliorejesha fomu za kuomba
kuteuliwa na chama hicho kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kabla ya
kikao cha Kamati Kuu, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye, alipotafutwa na NIPASHE jana kwa njia ya simu kutoa ufafanuzi
iwapo kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili kilifanyika kama ilivyokuwa
imepangwa awali, alisema: “Nianze na hili la Kamati Kuu (CC), mimi pia
sijui kinafanyika wapi na saa ngapi. Halafu hata hicho kikao cha Kamati
ya Usalama na Maadili unachoniuliza hapa; hakikufanyika.”
Kabla ya
Rais Kikwete kuongoza Kikao cha Kamati Kuu kwa ajili ya kufyeka majina
33 ya wagombea wanaoomba kuteuliwa kuwania kiti cha urais na kubaki
matano; alifanya kazi kubwa mbili katika siku ya jana, ikiwamo kuzindua
jengo jipya na la kisasa la CCM, maarufu kama Dodoma Convention Centre
na baadaye jioni kwenda kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Jumla ya makada 42 wa CCM walichukua fomu kwa ajili kuomba ridhaa kwa chama hicho kiwateue kuwania urais.
Hata hivyo, kati hao 42, makada 38 ndiyo waliorejesha fomu huku wanne `wakiingia mitini’ na fomu hizo.
NIPASHE
Maoni
Chapisha Maoni