LOWASSA AWATIBUA WAANDISHI WA HABARI
Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo hii Edward Lowassa amewakera waandishi wa habari baada ya kuwaita nyumbani kwake Masaki.
Taarifa iliyotumwa kwa wahariri leo asubuhi ilikuwa inasema:
Habari za asubuhi wahariri, Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa ana Press Conference
leo Saa 5:00 nyumbani kwake Masaki.
Mnaombwa kutuma waandishi wa habari na kwa wale wenye fursa kufika. Good morning.
Lakini baada ya waandishi kufika nyumbani kwake wakakutana na tangazo
kuwa kuwa ameahirisha kuzungumza na waandishi hadi hapo itakapo tangazwa
tena.
Kitendo hicho kimewakera sana waandishi wa habari.
Maoni
Chapisha Maoni