NIMECHOKA NA SITAKI KUITWA FISADI ASEMA LOWASSA ATAKA MWENYE USHAHIDI AJITOKEZE
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana aliwataka wanaomhusisha na ufisadi kuacha mara moja kwa sababu hakuna hata chembe ya ukweli katika tuhuma hizo.
Lowassa,
aliyeonekana kuzungumza kwa hisia, alisema hayo jana mara baada ya
kurejesha fomu ya kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Mbunge
huyo wa Monduli alikuwa mmoja kati ya makada tisa waliorudisha fomu
jana, ikiwa ni siku moja kabla ya kuisha kwa muda uliowekwa na chama
hicho.
Wengine
waliorejesha fomu jana ni Elidephonce Bilohe, Mwigulu Nchemba, Luhaga
Mpina, Dk Hamisi Kigwangalla, Hassy Kitine, Mariki Marupu, Dk Asha Rose
Migiro na Lazaro Nyalandu.
Hadi
sasa, tayari wanachama 32 kati ya 42 wa CCM walioomba kuteuliwa na
chama hicho kugombea urais wamerudisha fomu na kazi hiyo itahitimishwa
leo.
Hakuna
mtu ambaye amejitokeza hadharani kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi, lakini
tuhuma hizo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, hasa
kutokana na mbunge huyo wa Monduli kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu mwaka
2008 baada ya kuibuka sakata la mkataba wa ufuaji umeme wa dharura
baina ya Serikali na Kampuni ya Richmond RDC ya Marekani ambayo
ilionekana haina uwezo.
Wakati huo, Lowassa alisema kwenye hotuba yake ya kujiuzulu kuwa amefanya uamuzi huo “ili
kuonyesha dhana ya uwajibikaji, lakini kutokubaliana na utaratibu
uliotumika wa kusema uongo ndani ya Bunge kwa kumsingizia mtu.”
Akizungumza
jana kwenye ofisi za makao makuu ya CCM, Lowassa alirudia wito wake wa
kutaka wenye ushahidi wa tuhuma hizo wajitokeze hadharani.
“Nataka
nitumie fursa hii kuwataka wale wote ambao wamekuwa wakinituhumu kwa
miaka kadhaa sasa na kunihusisha na suala zima la rushwa, nawaambia
waache mara moja, kwani hakuna chembe hata ya ukweli wa maneno hayo,” alisema.
“Natoa
changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi wa tuhuma hizo za kipuuzi, autoe
na aeleze kwa ushahidi rushwa yoyote inayonihusu, aseme nimechukua lini,
kwa nani, kwa lipi na kiasi gani?”
Alisema
yeye ni mwadilifu na anaposema atasimamia vita dhidi ya rushwa atafanya
hivyo kwa vitendo bila kumuonea mtu na bila kumuonea haya yeyote.
“Ndugu
wanachama wenzangu na wananchi kwa jumla, ni lazima sasa tufike mahali
tuseme imetosha. Majungu yametosha, upotoshwaji umetosha, rushwa
imetosha na kwa pamoja tunaweza kukomesha haya. Tutayakomesha kwa
kusimamia ukweli, uadilifu, uaminifu na kutenda kwa haki,” alisema.
Alisema tuhuma hizo zimeendelea hata wakati wa kutafuta wadhamini kwa baadhi ya watu kuzieneza.
“Tumefanya kazi ya kutafuta na kuomba udhamini kwa uadilifu na umakini mkubwa. Na hapa nitumie nafasi hii pia kuwashukuru makatibu na viongozi wote wa Chama katika mikoa na wilaya kwa maandalizi mazuri katika kuifanikisha zoezi hili,” alisisitiza.
Alisema kuwa walifanya kazi yao vizuri kinyume kabisa cha vijimaneno vilivyoenezwa kwamba kulikuwa na matumizi ya fedha katika kuwatafuta wadhamni.
“Hivi kweli, unahongaje watu zaidi ya laki nane?” alihoji.
Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli, alisema tuhuma hizo zimekuwa zikitolewa na watu ambao wamekosa hoja na zinatolewa bila ushahidi wowote.
Alisema akifanikiwa kushika wadhifa wa urais, ataendesha nchi kwa kufuata katiba na sheria.
Kuhusu safari ya kusaka wadhamini, Lowassa aliwashukuru wana-CCM waliomdhamini na kwamba walijitokeza kwa wingi jambo ambalo limempa picha ya kuungwa mkono na kukubalika.
Alisema wanachama waliojitokeza kumdhamini walifanya hivyo kwa utashi wao na bila kishawishi chochote cha fedha au fadhila nyingine yoyote.
Alisema kuwa udhamini alioupata ni kielelezo cha vitendo kwamba wapo naye katika Safari ya Matumaini.
“Nina matumaini na imani kubwa kwamba mtaendelea kuniunga mkono ndani ya Chamna chetu ili kwa pamoja na mshikamano ndani ya Chama niweze kuteuliwa kugombea kiti cha urais,” alisema.
Lowassa alisema: “Kwa mafanikio haya ya hatua ya awali nina imani kwamba ni ishara njema kueleke hatua zilizobakia na uweza wake Mwenyezi Mungu Mungu, na kwa ushirikiano wenu kwa pamoja tutalivuka daraja ili hatimaye niwatumikie kwa utumishi uliotukuka nikiwa Rais wa Awamu ya Tano.”
Aliongeza kuwa: “Nina shauku kubwa ya kuunganisha nguvu na uwezo ya kila Mtanzania katika kupambana na umasikini wa nchi hii. Umasikini wa watu wetu siyo amri ya Mwenyenzi Mungu. Nina imani kabisa kwa pamoja tunaweza kutumia rasilimali tulizo nazo kwa bidii, maarifa na ufanisi zaidi ili kutokomeza umasikini huu.”

Ukumbi
wa Whitehouse, jana ulijaa wana-CCM ambao walifika kushuhudia Lowassa
akirudisha fomu tofauti na idadi iliyowahi kutokea kwa wagombea wengine
kadhaa waliomtangulia.
Hali
hiyo ilisababisha foleni kwenye Barabara ya Mtaa wa Kuu unaopita mbele
ya ofisi za CCM, na kusababisha usumbufu kwa wapita njia.
Lowassa
alifika akiwa ameongozana na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge
Ngombale Mwiru na wenyeviti wa chama hicho wa mikoa kadhaa pamoja na
wabunge.
Wabunge
hao ni Andrew Chenge (Bariadi Magharibi), Peter Serukamba (Kigoma
Mjini), Diana Chilolo (Viti Maalumu), Profesa Juma Kapuya (Urambo
Magharibi), Mary Chitanda (Viti Maalumu), Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,
Dk Makongoro Mahanga na Mary Mwanjelwa (Viti Maalumu).
Maoni
Chapisha Maoni