HIVI NDIVYO ARGENTINA WALIVYOPOKONYWA UBINGWA WA COPA AMERICA! MESSI ATOA MACHOZI KULIKOSESHA TAIFA LAKE UBINGWA ZAIDI YA MIAKA 20
Chile ndio mabingwa wa Copa America
Chile imewashinda Argentina kupitia kwa mikwaju ya penalti na kushinda kombe kubwa zaidi kati ya nchi za Marekani ya kusini la Copa Amerika.
Chile ambayo ni waandalizi waliwashinda Argentina mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu zote kukosa kufunga.
Mchezaji wa Arsenal Alexis Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain kupiga nje huku mkwaju wa Ever Banega ukinyakwa na kipa Claudio Bravo.
Awali Higuain alikuwa amekosa bao la wazi aliposalia na kipa baada ya dakika 90 za mchezo.
Sanchez karibia afunge katika dakika za ziada.
Miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliojaa kuishabikia timu yao ni wachimba mgodi 33 waliokwama chini ya mgodi kwa wiki kadhaa mwaka 2010,katika kisa kilichovutia hisia nyingi duniani.
Maoni
Chapisha Maoni