MWANASOKA MTANZANIA ATAMBULISHWA RASMI KLABU YA UJERUMANI


IMG-20150709-WA0028
Mugeta (wa kwanza kushoto)
Kijana wa Kitanzania Emily Mugeta ametambulishwa katika  timu yake mpya ya Neckarsulm Union Sports yenye makazi yake mjini, Neckarsulm nchini Ujerumani.
Timu hiyo inacheza ligi ya Verbandsliga ambayo ni miongoni mwa ligi za Ujerumani ambazo zina majina tofauti kama vile Bundesliga, second Bundesliga, Third Bundesliga.
Ili kuingia Verbandsliga unatakiwa kupitia kwanza Oberliga.
Wakwanza kushoto ni kocha wa timu hiyo, Torsten Damm anayemfuatia ni Mugeta
Mugeta amepigwa picha hizi juzi walipoanza mazoezi ambapo  wanajiandaa na mechi ya kutambulishwa rasmi kwa timu nzima ambayo watachuana na Hoffeinheim Julai 15 mwaka huu.
Kila la kheri Mugeta katika maisha yako ya soka huko Ujerumani, bila shaka utaiwakilisha vyema Tanzania.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA