MAREKANI MABINGWA WA KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE;


Marekani imenyakua Kombe la Dunia la Wanawake baada ya kuwazaba mabingwa watetezi Japan mabao matano kwa mawili. Ushindi huo ni wa kulipiza kisasi dhidi ya Japan
Miongoni mwa mashabiki 53,341 waliofika uwanjani kutizama fainali hiyo ni Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe.
Rais wa FIFA Sepp Blatter hakuhudhuria fainali hiyo kutokana na uchunguzi wa ufisadi unaoendeshwa na Marekani dhidi ya maafisa wakuu wa shirikisho hilo. Makamu wa Rais wa FIFA Issa Hayatou wa Cameroon, ambaye ni kiongozi wa Shirikisho la Kandanda Afrika – CAF ndiye aliyewakabidhi washindi Marekani Kombe la Dunia.
Mchezaji wa Marekani Carli Lloyd ameandikwa katika vitambu vya historia kama mwanamke wa kwanza kufunga mabao matatu katika fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake. Marekani ambayo ilishinda Kombe hilo mwaka wa 1991 na 1999, sasa ni taifa la kwanza kushinda taji hilo mara tatu. Fainali ya leo ilikuwa marudio ya mwaka wa 2011 nchini Ujerumani ambapo Japan ilipata ushindi kupitia mikwaju ya penalti. Taji hilo lilikuwa lao la kwanza la dunia katika historia ya nchi hiyo na lilikuja wakati nchi hiyo ilikuwa imeathirika na janga kubwa la tetemeko la ardhi na Tsunami.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA