EDWARD LOWASSA AKWATWA! HALI NI NGUMU KWA WALIOKATWA. SOMA HAPA.
“Anakatwa,
hakatwi” ndilo swali lililokuwa linaulizwa nchi nzima jana, lakini
hatimaye Kamati Kuu ya CCM iliyokutana hadi usiku wa manane iliibuka na
jibu kwamba Edward Lowassa amekatwa, huku kukiwa na wingu zito baada ya
wajumbe watatu kupingana na uamuzi huo.Muda
mfupi baada ya kikao hicho, pamoja na kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi
wa CCM, Nape Nnauye alikataa kutaja majina yaliyopitishwa, akaunti ya
Twitter ya CCM, iliwataja waliopitishwa kuwa ni Bernard Membe, Dk John
Magufuli, Dk Asha Rose Migiro, January Makamba na Amina Salum Ali na
kuwatupa wengine 33 akiwamo Lowassa.“Kikao
cha Kamati Kuu kimeisha salama. Kesho (leo) Halmashauri Kuu itakutana
kuanzia saa 4:00 asubuhi,” alisema Nape baada ya kikao hicho.Alipotakiwa
kutaja majina ya makada watano waliopitishwa, Nape alisema: “Nimeambiwa
mchakato bado unaendelea na kesho (leo) Halmashauri Kuu itakutana
kuendelea na kazi. Kwa hiyo nawakaribisha kesho kuanzia saa 4:00 asubuhi
mje mchukue picha, habari, karibu sana.” Mkutano Mkuu utafanyika saa
nane mchana leo.”
BONYEZA KUSOMA YOTE
BONYEZA KUSOMA YOTE
Maoni
Chapisha Maoni