TUNDU LISU AWEKWA MTU KATI BUNGENI
Ni baada ya kuomba
Mwongozo kuhusu swala lililoleta utata kwa siku kadha kuhusu uhalali wa
serikali kuwasilisha mpango wa mwaka mmoja badala ya miaka mitano.
Awali akiomba Mwongozo
mh.Lissu alisema serikali imekiuka kuleta mpango wa mwaka mmoja badala
ya miaka mitano ambayo ndio desturi ya mabunge yote yaliyopita na
kumtaka Spika kutokubali kuruhusu bunge lake tukufu kukiuka kanuni zake
kwa faida ya serikali. Huku akiendelea na kibwagizo cha hapa kazi tu
hapa kazi tu.
Kwa kukazia ndipo
akasimama Mh.Zitto na kuikumbusha serikali kuwa serikali ilikuwa na
uwezo kuwasilisha hoja ili kanuni zitenguliwe na mpango wa mwaka moja
ujadiliwe na kanuni zinaruhusu utenguaji huo.
Ndipo aliposimama Waziri
na kusema kuhusu suala la utenguaji wa kanuni serikali ilishakaa na
kamati ya kanuni ambapo kiongozi wa KUB alishiriki kwa kutuma
mwakilishi, na Mwakilishi mwenyewe alikuwa Lissu.
Waziri akasema
anamshangaa Lissu kwa kuomba mwongozo jambo ambalo alishiriki kutoa
maamuzi na akasema anaweza kutaja hata majina ya wajumbe wote
walioshiriki huo uamuzi.
NB. Wabunge waache unafiki na kuwa vigeugeu kwa kutafuta umaarufu usio na tija
Maoni
Chapisha Maoni