Huu ndo Mshahara na Posho anazolipwa Rais Barack Obama

Moja kati ya vitendawili ambayo wananchi wengi hujiuliza ni pamoja na kiasi ambacho mkuu wa nchi analipwa kama ujira wa kuwatumikia, kiasi kinachotolewa kwenye kodi zao.
Kwa nchi nyingi za Afrika, kufahamu kipato cha Rais wa nchi mara nyingi huwa kitendawili zaidi na hutia shaka zaidi pale marais wa baadhi ya nchi hizo wanapoonekana kuneemeka kupita kiasi na utumishi wa umma.
Hii ni tofauti kwa nchi ya Marekani ambapo mshahara na posho ya Rais huwekwa hadharani, na kiasi anachoingiza kwa mwaka hata kwa kazi zake binafsi pia sio siri. Husambazwa kama habari ya kawaida tu.
Rais wa Marekani, taifa lenye nguvu zaidi kiuchumi duniani likichuana na China, hulipwa mshahara wa $400,000 (sawa na shilingi za Tanzania 877,040,000) kwa mwaka.
Lakini, hupokea mshahara wake kwa mwezi hivyo ikijumlishwa hufikia kiasi hicho kwa mwaka.
Obama na Meza
Mbali na kiasi hicho cha mshahara wa mwaka, Obama hupata posho ya $50,000 kwa mwaka.
Hicho ndicho kiasi pekee anachopata Rais Obama kutoka serikalini kwa mwaka.
Pamoja na kiasi hicho, Rais wa Marekani hufaidi matunda ya kazi yake kwa kupewa ulinzi bure, kuishi Ikulu bure, usafiri wa Air Force One na huduma nyingine ndogondogo pamoja na familia yake.
Mke wa Rais, hana fungu lolote serikalini kupitia mgongo wa kuwa ‘First Lady’.
Hata hivyo, Obama amekuwa mchapakazi na amewekeza katika masuala mbalimbali pamoja na kuandika vitabu mbalimbali anavyoviuza, kama kazi yake ya pembeni isiyohusiana na majukumu yake kama Rais. Kazi hizo zimemsaidia kupata kiasi fulani cha fedha.
Mwaka 2011, ukishumlisha mshahara, posho na kazi zake hizo za nje, Obama alitajwa kuwa aliingiza kiasi cha $790,000.
Chanzo: Reuters

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA