JANGILI ALIYETUNGUA HELKOPTA SEREGENTI HUYU HAPA, MCHEKI NA INTEREJENSIA WA NGORONGORO ALIYERATIBU TUKIO HILO.
Njile Gonga (28) Huyu ndiye Jangili anadaiwa kutungua helkopta katika pori la Akiba la Maswa lililopo katika Wilaya ya Meatu Mkoani, ambapo katika tukio hilo rubani wa helkopta hiyo Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo.
Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha Interejensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa kiunganishi Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo. |
Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa imehimarsihwa mahakamani pamoja na kituo cha polisi Bariadi leo hii. |
Watuhumiwa wakiwa ndani ya gari la polisi, baada ya kufikishwa kituo cha polisi Bariadi wakitokea wilayani Meatu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani. |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Elaston Mbwilo akionyeshwa watuhumiwa wa ujangili ambao walihusika kutungua Helkopta. |
Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha Interejensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa kiunganishi Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo. |
Watuhumiwa wakiwa Mahakamani. |
Hii ni kama haijawahi kutokea kwa wakazi wa Mji wa Bariadi, Kwa mara ya kwanza kufurika katika viwanja vya Mahakama ya wilaya hiyo kushuhudia watuhumiwa hao. |
Watuhumiwa
wa tukio la kutungua ndege aina ya Helkopta na kumuua rubani wake Rodgers Gower
(37) raia wa uingereza lilitokea mnamo tarehe 29/01/2016 katika pori la akiba
Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, leo (jana) wamefikishwa mahakani kusomewa
mastaka yanayowakabili.
Watuhumiwa
hao walifikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Simiyu, chini ya ulinzi wa mkali wa
askari polisi, huku umati mkubwa wa wananchi wa mji wa bariadi waifurika
kushuhudia watuhumiwa hao.
Akiwasomea
mashtaka watuhumiwa hao Wakili mwandamizi wa serikali Mkoa wa Simiyu Yamiko
Mlekano alisema kuwa washitakiwa wote 9 wanakabiliwa na kesi tatu ambazo ni
Uhujumu uchumi, mauaji pamoja na umiliki wa siraha bila ya kibali cha serikali
zenye mashtaka tofauti.
Katika
kesi ya Uhujumu uchumi iliyosomwa chini ya Hakimu mkazi mfawidhi mwandamizi wa
mahakama hiyo John Nkwabi katika shtaka la kwanza mtuhumiwa namba moja Iddy
Mashaka (49) anatuhumiwa kujihusisha na kuratibu tukio la uhujumu uchumi
kinyume na kifungu 4(1)(d) sura (57) (1) na 60 (2) cha makosa ya uhujumu uchumi
sheria namba 200 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mlekano
alisema kuwa katika kosa hilo mshitakiwa kati ya tarehe 6 januari na 1/02/2016
katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu aliwashauri Mshitakiwa namba mbili Shija
Mjika (38) kuua wanayama wasiyoruhisiwa kama tembo.
Katika
shtaka la pili wakili huyo aliwataja watuhumiwa namba mbili hadi tisa ambao ni
Shija Mjika (38) Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42) Moses Mandagu (48) Dotto
Huya (45), Mwigulu Kanga (40) Mapolu Njige (50) pamoja na Mange Barumu (47),
watuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
Katika
shtaka hilo wakili aliieleza mahakama kuwa kati ya tarehe 21/01/2016 na
29/01/2016 katika wilaya ya Meatu, watuhumiwa hao walipanga na kuratibu tukio
la kuwinda wanyama aina ya tembo bila ya kibali cha serikali.
Hata
hivyo wakili huyo alieleza kuwa katika shtaka la tatu watuhumiwa namba mbili
hadi tisa waliotajwa hapo mwanzo, watuhumiwa kujihusisha na uwindaji wa wanyama
wasiyoruhusiwa kinyume na kifungu 47(a)(aa) cha sheria namba 5 ya mwaka 2009
sambamba na sura 14 (a) na kifungu 57 (1) cha uhujumu uchumi sura 200
iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Alisema
katika shataka hilo mnamo kati ya tarehe 26/01/2016 na 29/01/2016 katika
hifadhi ya Mwiba katika kijiji cha Makao wilayani Meatu watuhumiwa walimuua
tembo mwenye dhamani ya shilingi Milion 32,891,100 bila ya kibali cha serikali.
Katika
shtaka la nne watuhumiwa namba mbili hadi tisa wanatuhumiwa kwa kosa la
kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria namba 86(1)(2)(b) cha uhuwifadhi
wa wanyama pori sheria No 5/2009 sambamba na sura ya 14(d) na sura 57(1) cha
uhujumu uchumi sura ya 200.
Katika
maelezo ya kosa hilo ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa kati ya
29/01/2016 na tarehe 6/02/2016 katika wilaya ya meatu mkoa wa simiyu
walikamatwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo yenye uzito wa kilo 31
yenye thamani Milioni 32,891,100 bila ya kibali cha serikali.
Katika
shtaka namba tano watuhumiwa namba moja na mbili ambao ni Iddy Mashaka (49)
pamoja na Shija Mjika (38) wanatuhumiwa na uuzaji wa nyara za serikali kinyume
na kifungu cha sheria 84(1) cha uhuwifadhi wa wanyama pori sheria No 5/2009
sambamba na sura ya 14(b) na sura 57(1) cha uhujumu uchumi sura ya 200.
Katika
kosa hilo wakili alisema kuwa kati ya tarehe 6/01/2016 na tarehe 1/02/2016
katika wilaya a Meatu Mkoani Simiyu, watuhumiwa walikamatwa wakiwa
wanajihusisha na uuzaji wa nyara za serikali bila ya kibali.
Hata
hivyo katika kesi namba mbili ya Mauaji wakili Mlekano aliiambia mahakama kuwa
watuhumiwa ambao ni Shija Mjika (38), Njile Gunga (28) Dotto Pangali ( 42)
pamoja na Moses Mandago (28) wanashtakiwa kwa kosa la mauaji kinyume che sheria
ya 196 na 197 cha kanuni ya adhabu namba 16 iliyofanyiwa mwaka 2002.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao mnamo tarehe 29/01/2016 katika hifadhi ya
Mwiba kijiji cha Makao wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu walimuua rubani wa ndege
aina ya helkopta rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza.
Katika
kesi zote Mbili kwa mujibu wa hakimu huyo alisema kuwa watuhumiwa hawatakiwi
kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi
hiyo, ambapo keshi hizo zilihairishwa mpaka terehe 24/02/2016 mpaka
zitakapotajwa tena.
Sambamba
na hayo katika kesi ya tatu ambayo ni kukutwa na siraha kinyume cha sheria na
pasipo leseni ilisikilizwa katika mahakama hiyo chini ya Hakimu mfawidhi wa
wilaya Bariadi Mary Mrio ambapo watuhumiwa walikabiliwa na mashitaka
matano
Watuhumiwa
hao ni Mange Buluma,Shija Mjika,Dotto PanganiNjile Ngunga,Moses Mandagu,Dotto
Huya na Mwigulu Kanga ambapo baadhi yao walikiri kumiliki siraha kinyume
cha sheria pamoja na riasi akiwemo njile aliyetungua helkopta hiyo.
Watuhumiwa
hao ambao Shija Mjika, Moses Mandagu, Njile Ngunga pamoja na Dotto Pangani
walikiri mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na siraha aina ya bunduki Riffle 303
Namba 06490 kinyume cha sheria pamoja na risasi mbili.
Hata
hivyo Njile Ngunga pamoja na Moses Mandagu walikiri pia katika shtaka la tatu,
nne pamoja na tano la kukutwa na siraha bila ya kibali, kumiliki risasi bila ya
kibali, pamoja na kumiliki tena risasi kinyume cha sheria huku wengine kati ya
hao wakikana makosa hayo.
Hata
hivyo mahakama haikuweza kutoa hukumu juu ya watuhumiwa hao waliokiri kutokana
na vielelezo kutokuwepo mahakamani hapo, ambapo kesi hiyo ilihairishwa mpaka
kesho (Leo).
Watuhumiwa
wote walirudishwa rumande.
Maoni
Chapisha Maoni