STAA ZARI AHOFIA KUISHI BONGO KISA UTAJIRI WAKE
Dar
es Salaam: Ubuyu! Tumbuatumbua ya majipu ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk.
John Pombe Magufuli ‘JPM’ inadaiwa kumtisha mwandani wa Mwanamuziki
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’
kuja kuishi Bongo ikidaiwa kisa ni utajiri mkubwa alionao wenye shaka
juu ya malipo ya ushuru na mapato.
Habari
kutoka kwenye chanzo cha ndani cha familia ya Diamond, zimeeleza kuwa
Zari alikuwa na mpango wa kuhamishia miradi na makazi yake rasmi Dar
mwanzoni mwa mwaka 2016 lakini ndoto hiyo inaonekana kuyeyuka.
Chanzo
hicho kilieleza kuwa, familia ya Diamond imekuwa ikimshinikiza jamaa
huyo amshawishi Zari kuwekeza Bongo lakini kwa sasa mpango huo umefutika
kwani mwanadada huyo anaogopa kutumbuliwa majipu.
“Unajua Zari anafuatilia kila kitu kinachoendelea nchini. Kwa hiyo
usidhani hajui mambo ya TRA (Mamlaka ya Mapato) yalivyochachamaa.
“Unajua anasema akihamia Bongo itabidi aingize nchini yale magari yake
ya kifahari anayotembelea akiwa Sauz (Afrika Kusini) au Uganda lakini
anahofia tumbua majipu ya Magufuli.
“Wewe fikiria kama lile Range
(Rover) la Wema (Sepetu) limekamatwa na TRA, itashindikana nini kukamata
Hummer au Lamborghini ya Zari?
“Nafikiri ishu ni utajiri wake.
Nilishasoma kwenye vyombo vya habari vya Uganda kuwa utajiri wake wa
ghafla umekuwa ukiibua sana maswali na yeye huwa hapendi kuzungumzia
vyanzo vya utajiri wake,” kilinyetisha chanzo chetu.
Baada
ya kumwagiwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alithibitisha kuwa kweli Zari
hayupo Bongo yupo Sauz hivyo alimsaka Diamond ambaye alikuwa na haya ya
kusema: “Zari ana miradi mingi, muda wa kuwekeza Bongo ukifika atakuja
kufanya hivyo.
uhusu mheshimiwa (Magufuli) mimi nampongeza kwa
kutumbua majipu kwa sababu tulikuwa tunahitaji kiongozi kama yeye,”
alisema Diamond na kuongeza kuwa mpango wa Zari wa kuja kuishi Dar upo
palepale
Maoni
Chapisha Maoni