NEY WA MITEGO AMPIGA BITI MRISHO MPOTO
Rapa
Nay wa Mitego amedai msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akiamua
kuingia kwenye muziki wa Hip Hop atakuwa hana mpinzani kutokana na uwezo
wake wa kuandika mashairi.
Akizungumza na Bongo5 Jumanne hii, Nay alisema ikitokea akaingia labda atashindanishwa na Fid Q.
“Kwa
sasa nasema Fid Q hana mwezake katika uandishi, lakini namuona Mrisho
Mpoto kama angeamua kuingia kwenye Hip Hop sijui utamshindanisha na
nani,” alisema Nay.
“Huyu
jamaa huwa nafikiria anaumiza kichwa kiasi gani kuandaa kazi yake,
anatumia akili nyingi sana ndio maana nasema kama akiingia kwenye muziki
wa Hip Hop atakuwa hana mpinzani,” aliongeza.
Aidha, Nay wa Mitego amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula, kwani anajipanga kuachia kazi mpya hivi karibuni.
Maoni
Chapisha Maoni