MESSI KUKUTANA NA MTOTO ALIEVUMA DUNIANI KWA PICHA YAKE YA JEZI YA MFUKO WA PLASTIKI!
MCHEZAJI
BORA DUNIANI ambae huchezea Klabu ya Spain Barcelona, Lionel Messi,
anatarajiwa kukutana na Mtoto wa Afghanistan ambae alipata umaarufu
Duniani baada ya kupigwa Picha akivaa Jezi iliyotengenezwa kienyeji kwa
Mfuko wa Plastiki wa Rangi za Argentina na Jina la Messi huku pia ikiwa
na Namba 10.Mtoto huyo mwenye Miaka Mitano aitwae Murtaza Ahmadi
anampenda mno Messi lakini Familia yake ya Kimaskini inayoishi Jimbo la
Ghazni Jirani na Mji Mkuu wa Afghanistan, Kabul, Nchi ambayo ina
misukosuko ya vita, haina uwezo wa kununua Jezi Orijino ya Staa huyo wa
Argentina.
Maoni
Chapisha Maoni